top of page

Mwandishi:

Mhariri:

Imeboreshwa:

ULY CLINIC

Dkt. Sospeter B, MD

31 Oktoba 2026, 15:23:37

Kung’oa jino kwa Mjamzito: Mwongozo kwa Wagonjwa na Wataalamu

Jibu kwa ufupi


Jibu kwa ufupi: Ndiyo, ni salama – mwambie daktari wa meno kuwa una mimba. Usisubiri hadi kujifungua ukiwa na maumivu au uvimbe. Soma Kuoza kwa meno.


Maelezo


Muda bora


  • Miezi 1–3: dharura zitibiwe; mengine yanaweza kusubiri kidogo.

  • Miezi 4–6: muda mzuri zaidi kwa matibabu ya kawaida.

  • Miezi 7–9: inawezekana; mama alale akiinamia upande wa kushoto kuepuka presha kushuka.


Dawa


  • Ganzi: lidocaine (± adrenalini) – chaguo la kwanza.

  • Maumivu: paracetamol; ibuprofen/aspirini ziepukwe hasa baada ya wiki 20.

  • Antibayotiki: amoxicillin, penicillin, clindamycin – salama; tetracycline na doxycycline – hapana (huathiri meno na mifupa ya mtoto).


Kwa nini usisubiri


  • Maambukizi ya jino huweza kuenea usoni, shingoni au damuni.

  • Magonjwa ya fizi yanahusishwa na kujifungua kabla ya wakati na mtoto kuzaliwa na uzito mdogo.


Kwa wataalamu


  • Wasiliana na mtoa huduma wa uzazi kama mama ana presha, kisukari au mimba yenye hatari.

  • Tumia kiwango kidogo kinachohitajika cha ganzi; epuka kulala chali muda mrefu.


Nini cha kufanya


  • Piga mswaki mara 2 kwa siku kwa dawa yenye fluoride; tumia uzi wa meno.

  • Baada ya kutapika – sukutua kwa maji, subiri dakika 30 kabla ya mswaki.

  • Punguza vitu vitamu.

  • Mwone daktari wa meno angalau mara moja wakati wa ujauzito.

  • Soma Meno kuuma ukinywa baridi.


Dalili za hatari


Hospitali mara moja ukiwa na:


  • Uso au shingo kuvimba, kushindwa kufungua mdomo au kumeza.

  • Homa na maumivu makali ya jino.

  • Damu isiyokoma baada ya kung'oa jino.


Lini umwone daktari



Maswali yanayoulizwa mara kwa mara


1. Mjamzito anaweza kung'olewa jino?

Ndiyo, kipindi chochote ikihitajika.

2. Ganzi ya meno ni salama?

Ndiyo, lidocaine ni salama.

3. X-ray ya meno itamdhuru mtoto?

Hapana, ikitumiwa kwa kinga.

4. Nimeze ibuprofen kwa maumivu ya jino?

Epuka, hasa baada ya wiki 20; tumia paracetamol.

5. Antibayotiki ipi ni salama?

Amoxicillin, penicillin au clindamycin.

6. Nisubiri nijifungue?

Hapana kama una maumivu au uvimbe.

7. Fizi zinatoka damu ujauzitoni, ni kawaida?

Ni kawaida kiasi; safisha vizuri na mwone daktari wa meno.

Imeandikwa:

2 Aprili 2026, 19:07:21

ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.

​

Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.

Rejea za mada hii:

  1. American College of Obstetricians and Gynecologists. Committee Opinion No. 569: Oral health care during pregnancy and through the lifespan. Obstet Gynecol. 2013;122(2 Pt 1):417–22 (reaffirmed 2022).

  2. Oral Health Care During Pregnancy Expert Workgroup. Oral health care during pregnancy: a national consensus statement. Washington, DC: National Maternal and Child Oral Health Resource Center; 2012.

  3. U.S. Food and Drug Administration. FDA recommends avoiding use of NSAIDs in pregnancy at 20 weeks or later. Silver Spring (MD): FDA; 2020.

bottom of page