top of page

Mwandishi:

Mhariri:

Imeboreshwa:

Dr.Sospeter Mangwella, MD

24 Agosti 2026, 03:43:22

Lenge la usaha

Lenge usaha hufahamika pia kama pustule aina ya jeraha la ngozi ambalo huonekana kama mwinuko mdogo juu ya ngozi wenye kioevu cha usaha ndani yake. Usaha huu unaweza kuwa ishara ya maambukizi ya bakteria, fangasi, au hata kuwa bila maambukizi kama inavyoonekana kwa baadhi ya wagonjwa wa soriasis ya kipistula


Muonekano lenge usaha

  • Lenge dogo lilioinuka juu ya ngozi

  • Rangi nyeupe, ya manjano au kijani hafifu

  • Hujazwa na usaha unaoonekana wazi

  • Huweza kuuma, kuwasha au kuwa laini kwa mguso


Visababishi vya lenge usaha

  1. Maambukizi ya bakteria – kama vile impetigo au folliculitis.

  2. Maambukizi ya fangasi – kama tinea sugu inayoweza kuambatana na pustule.

  3. Soriasis ya pustul – hali ya kinga ya mwili inayosababisha upele wenye usaha bila maambukizi.

  4. Acne vulgaris – chunusi zinazojitokeza na usaha.

  5. Hali zingine za kinga – kama vile Michomokinga ya vena na lupas.


Utambuzi

  • Hutegemea muonekano wa kliniki

  • Uchunguzi wa usaha (Kuotesha vimelea)

  • Biopsy ya ngozi (kwa magonjwa yasiyo ya maambukizi)

  • Kipimo cha ngozi (skin scraping kwa fangasi)


Tiba

  • Maambukizi ya bakteria – hutibiwa kwa antibioticki ya kupaka au ya kumeza.

  • Pustule zisizoambukiza – hupatiwa dawa za kupunguza uvimbe (kama kortikosteroid ya akupaka au immunomodulator).

  • Kujitibu nyumbani – usafi wa ngozi, epuka kukwangua au kubinya pustul, tumia antiseptiki nyepesi.


Hitimisho

Pustule ni jeraha la kawaida linaloweza kuwa na chanzo tofauti. Ni muhimu kutambua iwapo kuna maambukizi au hali nyingine ya ngozi ili kutoa matibabu sahihi na kuzuia madhara ya muda mrefu.


Rejea za mada hii
  1. James WD, Berger TG, Elston DM. Andrews’ Diseases of the Skin: Clinical Dermatology. 13th ed. Philadelphia: Elsevier; 2019.

  2. Habif TP. Clinical Dermatology: A Color Guide to Diagnosis and Therapy. 6th ed. Elsevier; 2015.

  3. Bolognia JL, Schaffer JV, Cerroni L. Dermatology. 4th ed. Elsevier; 2017.

  4. Korman NJ. Management of psoriasis as a systemic disease: what is the evidence? Br J Dermatol. 2020;182(4):840-848. doi:10.1111/bjd.18123

  5. World Health Organization. Skin conditions. [Internet]. 2023 [cited 2025 Jun 17]. Available from: https://www.who.int/news-room/fact-sheets/detail/skin-diseases

Imeandikwa:

2 Aprili 2026, 17:08:28

ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.

​

Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.

Rejea za mada hii:

bottom of page