Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:
Dkt. Mangwella S, MD
Dkt. Benjamin L, MD
31 Oktoba 2026, 15:23:37

Matibabu ya dalili Kiasi za UVIKO-19
Jibu kwa ufupi
Jibu kwa ufupi: Pumzika, kunywa maji, paracetamol kwa homa, jitenge na wengine. Usinunue antibayotiki wala mchanganyiko wa vitamini. Una hatari kubwa au dalili za hatari – kituo cha afya. Soma COVID-19: dalili, vipimo na huduma ya nyumbani.
Maelezo
Huduma ya nyumbani (dalili kiasi)
Paracetamol kwa homa na maumivu.
Maji, supu, uji – kunywa mara nyingi.
Kula vyakula vya kawaida vyenye matunda na mboga.
Lala ubavu au tumbo kama kupumua ni kugumu kidogo.
Asali na maji ya uvuguvugu kwa kikohozi (si kwa mtoto chini ya mwaka 1).
Dawa zisizoshauriwa
Antibayotiki (azithromycin, amoxicillin) – hazitibu virusi; huongeza usugu.
Aspirini – haina faida; huongeza kuvuja damu.
Vitamini C, D, zinki kama tiba – hazijaonyesha kupunguza ugonjwa.
Ivermectin, hydroxychloroquine, dawa za kienyeji zisizothibitishwa.
Wenye hatari kubwa
Umri zaidi ya miaka 60, kisukari, presha, ugonjwa wa moyo, figo, mapafu, VVU isiyodhibitiwa, wasiochanjwa.
Dawa za kuzuia virusi (kama nirmatrelvir/ritonavir) hufanya kazi zaidi zikianzwa ndani ya siku 5 – kwa maelekezo ya daktari.
Nini cha kufanya
Jitenge na wengine hadi siku 3 hadi 5 baada ya homa kuisha na dalili kupungua; vaa barakoa ukikaa na watu.
Nawa mikono; fungua madirisha – soma Kujikinga na COVID-19.
Pima oksijeni kwa kifaa cha kidole kama kinapatikana.
Pata chanjo – soma Chanjo ya COVID-19.
Dalili za hatari
Hospitali mara moja ukiwa na:
Kupumua kwa shida au haraka; oksijeni chini ya 94%.
Maumivu ya kifua yasiyoisha.
Kuchanganyikiwa, kusinzia sana, midomo kuwa bluu.
Kushindwa kunywa au kula.
Lini umwone daktari
Dalili zaidi ya siku 7 au zinaongezeka.
Una hatari kubwa – mwone daktari mapema.
Homa inarudi baada ya kupungua.
Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
1. UVIKO-19 dalili kiasi hutibiwaje?
Kupumzika, maji, paracetamol, kujitenga.
2. Azithromycin inatibu UVIKO-19?
Hapana.
3. Vitamini C na zinki zinasaidia?
Hazijaonyesha faida kama tiba.
4. Aspirini inafaa?
Hapana kwa UVIKO-19 dalili kiasi.
5. Nani anahitaji dawa za kuzuia virusi?
Wenye hatari kubwa, ndani ya siku 5, kwa daktari.
6. Nijitenge kwa muda gani?
Hadi siku 3 hadi 5 baada ya homa kuisha na dalili kupungua.
Imeandikwa:
2 Aprili 2026, 19:17:50
ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.
Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.
Rejea za mada hii:
World Health Organization. Therapeutics and COVID-19: living guideline. Geneva: WHO; 2023.
World Health Organization. Clinical management of COVID-19: living guideline. Geneva: WHO; 2023.
Ministry of Health, United Republic of Tanzania. Standard Treatment Guidelines and National Essential Medicines List (STG/NEMLIT), 7th edition. Dodoma: Ministry of Health; 2026.

