top of page

Mwandishi:

Mhariri:

Imeboreshwa:

ULY CLINIC

ULY CLINIC

31 Oktoba 2026, 15:23:37

Ninapokojoa mwishoni mwa mkojo unatoka uchafu kidogo kama usaha, shida ni nini?

Jibu kwa ufupi


Jibu kwa ufupi: Nenda kituo cha afya upimwe na kutibiwa pamoja na mwenzi wako; usinunue antibayotiki dukani. Soma Uume kutoa usaha na kuvimba.


Maelezo


Visababishi


  • Kisonono – usaha mzito wa njano/kijani, kuungua sana; soma Kisonono.

  • Klamidia na mycoplasma – uchafu mwepesi, kuungua kidogo, mara nyingi asubuhi; soma Klamidia.

  • Trikomona – uchafu kidogo, muwasho.

  • Prostatitis – maumivu ya kinena, kumwaga kwa maumivu, homa; soma Prostaitisi.

  • UTI – kukojoa mara kwa mara, mkojo wenye harufu.


Dalili zinazoambatana


  • Kuungua au maumivu ukikojoa.

  • Muwasho ndani ya uume.

  • Korodani kuuma au kuvimba.

  • Mara nyingi hakuna dalili nyingine.


Nini cha kufanya



Dalili za hatari


  • Homa, korodani kuvimba ghafla, kushindwa kukojoa – kituo cha afya mara moja.


Lini umwone daktari


  • Usaha au uchafu wowote kutoka uumeni.

  • Dalili zimerudi baada ya matibabu – soma Madhara ya kutotibu usaha.

  • Damu kwenye mkojo au shahawa.


Maswali yanayoulizwa mara kwa mara


1. Usaha mwishoni mwa mkojo ni gono?

Mara nyingi kisonono au klamidia; pima.

2. Naweza kununua dawa dukani?

Hapana; dawa sahihi na mwenzi kutibiwa ni muhimu.

3. Mwenzi wangu hana dalili, atibiwe?

Ndiyo.

4. Prostatitis inaleta usaha?

Wakati mwingine, pamoja na maumivu ya kinena.

5. Usipotibiwa kuna madhara?

Ndiyo – korodani kuvimba, mrija kubana, ugumba.

6. Lini nirudi kwenye ngono?

Siku 7 baada ya wote kumaliza dawa.

Imeandikwa:

2 Aprili 2026, 17:07:10

ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.

​

Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.

Rejea za mada hii:

  1. Ministry of Health, United Republic of Tanzania. Standard Treatment Guidelines and National Essential Medicines List (STG/NEMLIT), 7th edition. Dodoma: Ministry of Health; 2026.

  2. Workowski KA, et al. Sexually Transmitted Infections Treatment Guidelines, 2021 – Urethritis. MMWR Recomm Rep. 2021;70(4).

  3. World Health Organization. Guidelines for the management of symptomatic sexually transmitted infections. Geneva: WHO; 2021.

bottom of page