top of page

Mwandishi:

Mhariri:

Imeboreshwa:

Dkt. Sospeter B, MD

Dkt. Salome A, MD

31 Oktoba 2026, 15:23:37

Presha ya kushuka matibababu ya nyumbani

Jibu kwa ufupi


Jibu kwa ufupi: Simama taratibu, kunywa maji ya kutosha, kula milo midogo, kaa au lala ukihisi kizunguzungu. Kuzimia au maumivu ya kifua – hospitali. Soma Shinikizo la chini la damu.


Maelezo


Aina na hatua


  • Kusimama haraka / asubuhi – kaa kitandani dakika 1–2, sogeza miguu, kisha simama taratibu; inua kichwa cha kitanda kidogo.

  • Maji kabla ya kuamka – glasi 1–2 za maji; tafiti ndogo zimeonyesha huinua presha kwa muda; tafiti kubwa zinahitajika.

  • Baada ya kula – milo midogo, wanga kidogo, pumzika baada ya kula; punguza pombe.

  • Mjamzito – lala kwa ubavu wa kushoto, si chali.

  • Upungufu wa damu – tibu chanzo; soma Dalili za awali za upungufu wa damu.


Kwa ushauri wa mtoa huduma


  • Chumvi zaidi kidogo – si kwa wenye ugonjwa wa moyo, figo au presha ya juu wakati mwingine.

  • Soksi za kubana miguu.

  • Kubadilisha dawa zinazoshusha presha.

  • Dawa za kuinua presha – kwa wachache.


Nini cha kufanya


  • Kunywa maji lita 1.5–2 kwa siku (isipokuwa ukishauriwa vinginevyo).

  • Epuka kusimama muda mrefu bila kusogeza miguu.

  • Mazoezi ya mara kwa mara huboresha mzunguko.

  • Andika presha na dalili; mpelekee mtoa huduma.

  • Soma Kizunguzungu.


Dalili za hatari


Hospitali mara moja ukiwa na:


  • Kuzimia, maumivu ya kifua, kushindwa kupumua.

  • Ngozi baridi, yenye jasho, mapigo ya moyo kwenda kasi na kuchanganyikiwa (mshtuko).

  • Kutokwa damu, kutapika au kuharisha sana.


Lini umwone daktari


  • Kizunguzungu cha mara kwa mara.

  • Kuanguka.

  • Dalili zilianza baada ya dawa mpya.

  • Una kisukari au ugonjwa wa moyo.


Maswali yanayoulizwa mara kwa mara


1. Presha ya chini ni kiasi gani?

Chini ya 90/60 mmHg.

2. Presha ya chini ni hatari?

Bila dalili mara nyingi hapana; yenye dalili ichunguzwe.

3. Nile chumvi zaidi?

Kwa ushauri wa mtoa huduma tu.

4. Kwa nini napata kizunguzungu nikisimama?

Presha hushuka ghafla – simama taratibu.

5. Mjamzito alale vipi?

Kwa ubavu wa kushoto.

6. Dawa zinaweza kushusha presha?

Ndiyo, baadhi – mwambie mtoa huduma.

Imeandikwa:

24 Agosti 2026, 03:58:12

ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.

​

Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.

Rejea za mada hii:

  1. Freeman R, et al. Consensus statement on the definition of orthostatic hypotension, neurally mediated syncope and the postural tachycardia syndrome. Clin Auton Res. 2011;21(2):69–72.

  2. Shibao C, Lipsitz LA, Biaggioni I. Evaluation and treatment of orthostatic hypotension. J Am Soc Hypertens. 2013;7(4):317–24.

  3. Jordan J, et al. Water drinking as a treatment for orthostatic syndromes. Am J Med. 2002;112(5):355–60.

  4. Ministry of Health, United Republic of Tanzania. Standard Treatment Guidelines and National Essential Medicines List (STG/NEMLIT), 7th edition. Dodoma: Ministry of Health; 2026.

bottom of page