top of page

Mwandishi:

Mhariri:

Imeboreshwa:

ULY CLINIC

Dkt. Helen L, M.D

31 Oktoba 2026, 15:23:37

Salmonella typhi husababisha taifod

Jibu kwa ufupi


Jibu kwa ufupi: Typhoid hutibika kwa antibayotiki sahihi kulingana na miongozo. Homa isiyoisha ichunguzwe kwa kuotesha damu, si Widal pekee. Soma Homa ya matumbo.


Maelezo


Dalili


  • Homa inayopanda taratibu siku kwa siku.

  • Kichwa kuuma, uchovu, kukosa hamu ya kula.

  • Maumivu ya tumbo, choo kigumu au kuharisha.

  • Mara chache vipele vidogo vya waridi tumboni.

  • Matatizo – utumbo kutoboka, damu tumboni (wiki ya 2 hadi 3).


Wabebaji


  • Hawana dalili lakini hutoa bakteria kwenye kinyesi.

  • Huwa zaidi kwa wenye mawe kwenye kibofu cha nyongo – soma Mawe kwenye kibofu cha nyongo.

  • Wanaohudumia chakula wapimwe na kutibiwa.


Vipimo


  • Kuotesha damu – bora wiki ya kwanza.

  • Kuotesha kinyesi – kwa wabebaji na wiki za baadaye.

  • Widal – hutoa majibu chanya mengi ya uongo; usitegemee peke yake.


Nini cha kufanya


  • Maliza antibayotiki zote kama ulivyoandikiwa; usinunue dawa bila uchunguzi – usugu umeongezeka.

  • Kunywa maji salama – soma Tumia maji safi.

  • Nawa mikono kwa sabuni baada ya choo na kabla ya kula.

  • Chanjo ya typhoid (TCV) – kwa watoto na wasafiri pale inapopatikana.

  • Kula chakula kilichopikwa kikiwa cha moto.


Dalili za hatari


Hospitali mara moja ukiwa na:


  • Maumivu makali ya tumbo ghafla, tumbo kuwa gumu.

  • Damu kwenye choo au choo cheusi.

  • Kuchanganyikiwa, kusinzia sana.

  • Kutapika kila kitu.


Lini umwone daktari


  • Homa zaidi ya siku 3.

  • Homa haishuki baada ya siku 3 za antibayotiki.

  • Umeambiwa una typhoid mara kwa mara kwa kipimo cha Widal.


Maswali yanayoulizwa mara kwa mara


1. Typhoid husababishwa na nini?

Salmonella Typhi; paratyphoid na Salmonella Paratyphi.

2. Kipimo cha Widal kinaaminika?

Hapana peke yake; kuotesha damu ni bora.

3. Typhoid inaweza kujirudia?

Ndiyo, au mtu kubaki mbebaji.

4. Mbebaji wa typhoid ni nani?

Mtu asiye na dalili anayetoa bakteria kwenye kinyesi.

5. Kuna chanjo ya typhoid?

Ndiyo, chanjo ya conjugate (TCV).

6. Typhoid inatibika?

Ndiyo, kwa antibayotiki sahihi.

Imeandikwa:

2 Aprili 2026, 19:17:50

ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.

​

Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.

Rejea za mada hii:

  1. Ministry of Health, United Republic of Tanzania. Standard Treatment Guidelines and National Essential Medicines List (STG/NEMLIT), 7th edition. Dodoma: Ministry of Health; 2026.

  2. World Health Organization. Typhoid – fact sheet. Geneva: WHO; 2023.

  3. World Health Organization. Typhoid vaccines: WHO position paper – March 2018. Wkly Epidemiol Rec. 2018;93(13):153–72.

bottom of page