top of page

Dalili na viashiria vya magonjwa mbalimbali

Unashauriwa kufuata ushauri wa daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma makala. Bofya picha au neno soma zaidi ili kuingia kwenye makala kwa undani.

Maumivu wakati wa kupitisha haja kubwa

Maumivu wakati wa kupitisha haja kubwa

Hisia za maumivu wakati wa kupitisha haja kubwa huwapata watu wengi duniani na mara nyingi husababishwa na hali au magonjwa yanayozuilika na kutibika mfano haja ngumu, mpasuko njia ya haja kubwa, bawasiri, kuchomoza kwa puru, kaswende, klamidia, kuhara, n.k. Upatwapo na dalili hii wasiliana na daktari kwa uchunguzi na tiba.

Kukojoa mara kwa mara usiku

Kukojoa mara kwa mara usiku

Tatizo la kukojoa mara kwa mara wakati wa usiku huongezeka kwa jinsi umri wa mtu unavyoongezeka kufikia mtu 1 kati ya 3 baada ya kutimiza miaka 30. Visababishi vikuu ni mwili kutengeneza mkojo mwingi wakati wote au usiku tu na uwezo mdogo wa kibofu kutunza au kutoa mkojo. Ongea na mtaalamu wa afya kupata tiba inayoendana na tatizo lako.

Hedhi yenye damu kidogo

Hedhi yenye damu kidogo

Kwa kawaida mwanamke hupoteza mililita 5 hadi 80 za damu kwenye kila hedhi kila mwezi. Kupoteza kiasi chini ya mililita 30 za damu kwa kila hedhi hufahamika kama hedhi yenye damu kidogo. Baadhi ya visababishi ni mvurugiko wa homoni, ujauzito, koma hedhi, msongo, dawa za uzazi wa mpango n.k.

Maumivu ya tumbo baada ya kutoa mimba

Maumivu ya tumbo baada ya kutoa mimba

Maumivu ya tumbo baada ya kutoa mimba kwa dawa au kusafishwa kizazi ni kawaida kudumu kwa muda wa siku 3 hadi wiki moja kabla ya kupotea. Endapo maumivu yanazidi au hayaishi baada ya muda huu na damu inaendelea kutoka, wasiliana na daktari wako kwa uchunguzi na tiba.

Hedhi baada ya kutoa mimba

Hedhi baada ya kutoa mimba

Hedhi kwa kawaida hurudi ndani ya wiki 4–6 kulingana na mwili wa mtu na kiwango cha homoni kurudia kawaida. Ikiwa hedhi haijarudi baada ya wiki 6–8 au kuna dalili zisizo za kawaida, ni vyema kumuona mtaalamu wa afya kwa uchunguzi.

bottom of page