top of page

Dalili na viashiria vya magonjwa mbalimbali

Unashauriwa kufuata ushauri wa daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma makala. Bofya picha au neno soma zaidi ili kuingia kwenye makala kwa undani.

Kutounga na kuunga vibaya kwa mifupa

Kutounga na kuunga vibaya kwa mifupa

Kutounga au kuunga vibaya kwa mifupa ni tatizo linalotokea sana duniani na huambatana na dalili mbalimbali. Makala hii imeelezea visababishi, vihatarishi, sehemu za mwili tatizo linapotokea sana na namna ya kujikinga na tatizo hili.

Dalili za Msongo

Dalili za Msongo

Msongo ni mchakato wa mwili kupoteza uwezo wa kubadilika ili kukabiliana na mabadiliko ya hali au mazingira, kiasi cha kupelekea mabadiliko ya kisaikolojia na kibiologia yanayochangia kusababisha magonjwa. Zuia msongo kwa kula vema, kufanya mazoezi na kulala muda wa kutosha, kuwa na malengo halisi na kupata ushauri wa daktari au viongozi wadini.

Kushuka kiwango cha sukari kwenye damu

Kushuka kiwango cha sukari kwenye damu

Kushuka kwa sukari mwilini (au kuishiwa na sukari) hufahamika kwa neno la kitatibu kama “hypoglycemia” lenye maana ya kushuka kwa kiwango cha sukari kwenye damu kwa kiwango ambacho si cha kawaida.

Aina za degedege

Aina za degedege

Degedege ni dalili inayoonesha mvurugiko katika mawasiliano ya umeme katika seli za ubongo
Hali hii huwapata watu wengi, inakadiriwa kuwa mtu mmoja kati ya kumi anaweza kupata degedege wakati wa maisha yake.

Maumivu ya koo

Maumivu ya koo

Maumivu ya koo ni dalili ya hisia za kuhisi maumivu, ukavu au kukwanguliwa kwa koo. Tatizo hili huwapata watu wengi duniani. Mara nyingi maumivu ya koo husababishwa na maambukizi ya virusi na hewa kavu kwenye mazingira na mara nyingi dalili hii hupotea yenyewe bila matibabu.

bottom of page