top of page

Dalili na viashiria vya magonjwa mbalimbali

Unashauriwa kufuata ushauri wa daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma makala. Bofya picha au neno soma zaidi ili kuingia kwenye makala kwa undani.

Msinyao wa urethra

Msinyao wa urethra

Msinyao wa urethra kitiba hufahamika kama ‘urethral stricture’ ni ugonjwa unaosababishwa na makovu au uvimbe katika kuta za mrija wa mkojo wenye jina la urethra. Kusinyaa huko husababisha mrija kuwa mwembamba hivyo kuleta dalili mbalimbali kama vile mkojo kushindwa kutoka, kutumia nguvu wakati wa kukojoa, kukojoa mara kwa mara, hisia za kutokojo mkojo wote na dalili zingine.

Michirizi ya mishipa ya damu kwenye

Michirizi ya mishipa ya damu kwenye

Tatizo la mwonekano wa michirizi ya mishipa ya damu kwenye ngozi katika makala hii imetumika kumaanisha tatizo lenye jina kitiba kama ‘Telangiectasia’

Syndrome ya Asherman

Syndrome ya Asherman

Syndrome ya asherman kwa jina jingine hufahamika kama makovu mshikamano ndani ya mfuko wa kizazi, au makovu ya Asherman hutokea pale endapo makovu yametengenezwa ndani ya kiwili cha kizazi pamoja na au maeneo ya ya shingo ya uzazi.

Maumivu ya misuli

Maumivu ya misuli

Maumivu ya misuli si ugonjwa bali ni hali au tatizo Fulani linaloendelea ndani ya mwili. Baadhi ya visababishi vikuu huwa ni mgandamizo, matumizi makubwa ya misuli, msongo wa misuli au ndani ya misuli.

Kutapika damu

Kutapika damu

Kutapika damu ni kitendo cha kutoa matapishi ya damu kutoka tumboni, hufahamika kwa jina la kitiba ‘hematemesis, na huashiria dalili ya tatizo fulani linaloendelea kwenye mfumo wa chakula.

bottom of page