top of page

Mwandishi:

Mhariri:

ULY CLINIC

Dkt. Sospeter B, MD

8 Februari 2021 19:18:15

Kutapika damu
shahawa-zenye-damu-ulyclinic-compressor.

Kutapika damu

Kutapika damu ni kitendo cha kutoa matapishi ya damu kutoka tumboni, hufahamika kwa jina la kitiba ‘hematemesis, na huashiria dalili ya tatizo fulani linaloendelea kwenye mfumo wa chakula. Ukipata matapishi yalichochanganyika na michirizi ya damu, tatizo hili huwa halina sifa ya kuitwa kutapika damu, bali huitwa kutapika matapishi yenye damu.


Kuna baadhi ya hali au magonjwa yanayoweza kupelekea kutapika damu au kutapika matapishi yenye damu. Kutapika matapishi yenye damu mara nyingi husababishw ana sababu za kawaida kama vile, matatizo ya fizi au majeraha ya fizi, kutapika damu uliyomeza kutoka puani, matatizo ya koo au tumbo.

Kutapika damu huweza kuambatana na dalili zingine kama vile kupata haja kubwa laini inayonata na yenye rangi nyeusi au kahawia.


Ukipata tatizo la kutapika damu, mara nyingi dalili hii humaanisha kuna tatizo kubwa linalohitaji matibabu ya haraka. Baadhi ya watu wanaotapika damu, visababishi huwa ni kuvia kwa damu ndani ya tumbo kutokana na vidonda vya tumbo, kupasuka kwa misipa ya damu n.k.


Visababishi


Hali na magonjwa yanayoweza kusababisha kutapika damu ni pamoja na;


 • Kufeli ghafla kwa Ini

 • Matumizi ya kupindukia ya dawa aspirini

 • Saratani ndani ya tumbo

 • Kusinyaa kwa ini kunakoweza kusababiswha na matumizi ya pombe kupita kiasi

 • Madhaifu kwenye mishipa ya damu ya tumbo

 • Kuchomoza kwa mishipa ya damu yaarteri ndani ya tumbo kitiba Dieulafoy's lesion

 • Tatizo la duodenitis

 • Saratani ya umio

 • Kutanuka kwa mishipa ya veini ya umio

 • Uvimbe kwenye mrija wa esophagas unaoweza kusababishwa na matumizi ya pombe kupita kiasi

 • Vidonda ndani ya tumbo au matumbo

 • Kutanuka kwa mishipa ya damu ndani ya tumbo

 • Kuchanika kwa mrija wa esophagus kunakosababishwa na kutapika au kukohoa sana. Kwa jina la kitiba ‘Mallory Weiss tear’

 • Matumizi ya kupindukia ya dawa za kupunguza maumivu jamii ya Nonsteroidal anti-inflammatory drugs

 • Saratani ya kongosho

 • Uvimbe kwenye tezi pancreas

 • Shinikizo la damu kwenye mishipa ya vein za portal

 • Kutapika kwa muda mrefu

 • Vidonda vya tumbo vinavyovuja damu kutoka tumboni au sehemu ya utumbo yenye jina la duodenum


Visababishi kwa watoto

Sababu zinazoweza kusababisha kutapika damu kwa watoto ni pamoja na;


 • Magonjwa ya kuzaliwa nayo

 • Madhaifu ya kuganda kwa damu

 • Mzio dhidi ya maziwa

 • Kumeza damu inayotoka puani

 • Kumeza kitu tumboni

 • Upungufu wa vitamin K


Wakati gani wa kupata msaada wa dharura?Endapo unatapika damu na unapata dalili zifuatazo ni vema ukapiga simu ya dharura ili kupatiwa msaada wa haraka


 • Kupumua haraka haraka bila kina

 • Kizunguzungu na kuhisi kichwa chepesi

 • Kuona ukungu

 • Kuzimia

 • Kukanganyikiwa

 • Kichefuchefu

 • Kuhisi unakuwa wa baridi

 • Kupunguza kiwango cha mkojo


Vipimo


Baadhi ya vipimo daktari wako anaweza pendekeza ufanye ili kutambua kisababishi au kufanya matibabu ni pamoja na


 • Kipimo cha CT scan

 • Kipimo cha endoscopy, kinachopitishwa mdomoni kuangalia ndani ya mfumo wa chakula

 • Kipimo cha ultrasound

 • Kipimo cha X-ray

 • Kipimo cha MRI

 • Kipimo cha utendaji kazi wa Ini (Liver function Test)

 • Kipimo cha wingi wa damu au picha nzima ya damu (Full blood picture)


Matibabu


Matibabu ya kutapika damu hutegemea kisababishi, matibabu ya ujumla huhusisha kuongezewa maji endapo umepoteza kiwango kikuba cha damu, kuongezewa damu.


Madhara


Madhara ya kutapika damu ni pamoja na;


 • Kuingia kwa matapishi ndani ya mfumo wa hewa- hii hupelekea kupata nimoni ya matapishi ya damu

 • Kuishiwa damu

 • Kuferi kwa ogani mbalimbali mwilini ikiwa pamoja na moyo

 • Kifo- endapo utapoteza damu nyingi


Kinga


Unaweza kujikinga kwa kujikinga na baadhi ya visababishi vinavyoweza kukupelekea kutapika damu kama vile


 • Kuacha kunywa pombe kupita kiasi

 • Kutibiwa vidonda vya tumbo

 • Kucha kutumia dawa za maumivu ya asprini au Jamii ya NSAIDs mara kwa mara

 • Kula kwa wakati ili kukinga na vidonda vya tumbo

 • Kuwa na tabia ya kujisomea kuhusu masuala mbalimbali ya kiafya na kinga

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii

Imeboreshwa, 

19 Julai 2023 19:54:12

Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini

[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]

Rejea za mada

1.National Institute of Diabetes and Digestive and Kidney Diseases. Gastrointestinal (GI) bleeding.https://www.niddk.nih.gov/health-information/digestive-diseases/gastrointestinal-bleeding. Imechukuliwa 08.02.2021

2.Douglas G, et al. The gastrointestinal system. In: Macleod's Clinical Examination. 13th ed. Philadelphia, Pa.: Elsevier. 2013. http://www.clinicalkey.com. Imechukuliwa 08.02.2021

3.Vomiting blood (haematemesis). National Health Service. http://www.nhs.uk/conditions/vomiting-blood/Pages/Introduction.aspx?print=636211396418352636. Imechukuliwa 08.02.2021

4.Rockey DC. Causes of upper gastrointestinal bleeding in adults. http://www.uptodate.com/home. Imechukuliwa 08.02.2021

5.Villa X. Approach to upper gastrointestinal bleeding in children. http://www.uptodate.com/home. Imechukuliwa 08.02.2021

6.Vomiting blood. https://my.clevelandclinic.org/health/symptoms/17708-vomiting-blood. Imechukuliwa 08.02.2021

7.Vomiting blood (haematemesis). https://www.nhs.uk/conditions/vomiting-blood/. Imechukuliwa 08.02.2021

8.I. Dodd Wilson. Hematemesis, Melena, and Hematochezia. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK411/. Imechukuliwa 08.02.2021

9.Prashanth Rawla, et al. Mallory Weiss Syndrome. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK538190/. Imechukuliwa

bottom of page