Dalili na viashiria vya magonjwa mbalimbali
Unashauriwa kufuata ushauri wa daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma makala. Bofya picha au neno soma zaidi ili kuingia kwenye makala kwa undani.

Kuganda kwa damu
Kuganda kwa damu ni moja ua njia za ulinzi wa mwili dhidi ya majeraha yanayotokea ndani na nje ya mwili, njia hii huzuia kiwango kikubwa cha damu kupotea na kuvilia ndani ya mwili. Chembe sahani za damu pamoja na protini mbalimbali zinazohusika na ugandishaji damu hushirikiana kwa karibu iki kufanya dmau igande baada ya kupata jeraha mwilini.

Kukauka kwa uke: Sababu, dalili Uchugnuzi na Tiba
Kukauka kwa uke (Kuwa na uke mkavu) ni tatizo linalofahamika sana na linaloweza kuwapata wanawake katika umri wowote ule, hata hivyo hutokea sana kwa wanawake wenye umri mkubwa(miaka kati ya 50-60) haswa katika kipindi cha komahedhi. Makala hii imezungumzia kwa ujumla sababu za uke mkavu pamoja na uke mkavu wakati wa ngono/kujamiana

Kujisaidia kinyesi chenye harufu mbaya
Haja kubwa au kinyesi kwa kawaida huwa na harufu i isiyopendeza watu wengi na wakati mwingine baadhi ya watu hukataa kabisa kuangalia kinyesi kwa sababu huweza kupata kichefuchefu au kutapia. Licha ya kuwa na harufu mbaya, kinyesi kinaweza kuwa na harufu mbaya Zaidi ya ile ambayo umeizoea. Makala hii imezungumzia sababu za kitaalamu za kupata kinyesi chenye harufu mbaya.


