Dalili na viashiria vya magonjwa mbalimbali
Unashauriwa kufuata ushauri wa daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma makala. Bofya picha au neno soma zaidi ili kuingia kwenye makala kwa undani.

Kuishiwa pumzi
Hali na magonjwa mbalimbali yanaweza kusababisha tatizo la kuishiwa pumzi. Mara nyingi kuishiwa pumzi hutokana na matatizo ya moyo na mapafu, moyo na mapafu huhusika kwenye uchukuaji na usafirishaji wa hewa safi ya oksijeni kwenda kwenye tishu mbalimbali na kuondoa hewa chafu ya kaboni monoksaidi kwenye damu.

Homon Imbalance: Dalili, Visabaishi, Uchunguzi na Tiba
Mvurugiko wa homoni unaweza kusababishwa na hali kama matatizo ya tezi ya shingo, ugonjwa wa polisistiki ovari, kisukari, msongo wa mawazo wa muda mrefu, uzito kupita kiasi, baadhi ya dawa na mabadiliko ya kawaida kama ujauzito au komahedhi. Kudhibiti uzito, kula mlo kamili, kufanya mazoezi, kupunguza msongo wa mawazo na kupata uchunguzi wa kitaalamu pale dalili zinapoendelea husaidia kurekebisha uwiano wa homoni na kulinda afya kwa ujumla.

Dalili ya mzio
Mzio hutokea wakati mfumo wa kinga za mwili unaitikia vitu vigeni vyote vinapoingia kwenye mwili, mfano sumu mbalimbali, harufu za maua na poleni au baadhi ya vyakula kwa baadhi ya watu. Mfumo huu wa kinga za mwili ni muhimu sana kwani husaidia kumlinda mtu na sumu/kemikali ambazo hazihitajiki mwilini.


