Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
27 Oktoba 2020 05:37:52
Dawa ya Cefazolin
Cefazolin ni aina ya dawa ambayo ipo kwenye kundi la kwanza la antibayotiki jamii ya Cephalosporin. Dawa hii hutumika kupambana na maambukizi mbalimbali kwenye mwili. Dawa hii huwa maarufu kwa majina ya Ancef na Kefzol
Rangi, uzito na fomu ya Cefazolin
Rangi ya dawa ni ya njano lakini mara nyingi hutegemea aina ya kiwanda kinachotengeneza Cefazolin hupatikana katika mfumo wa unga ambao huandaliwa kwa ajili ya sindano wenye uzito wa; • 500 mg • 1 g • 2 g • 10 g • 20 g • 100 g • 200 g
Namna Cefazolin inavyofanya kazi
Dawa hii hufanya kazi kwa kuzuia ukuaji wa bakteria kwa kuzuia utengenezaji wa peptidoglacan ambayo huunda ukuta wa seli kwenye bakteria ,Kwa kufanya hivyo hupelekea kufa kwa bakteria
Dawa zilizo kundi moja na Cefazolin
Dawa zingine zilizo kwenye kundi moja la Cephalosporin ya kwanza ni ;
• Cefadroxil • Cephalexin • Cephalothin • Cephapirin • Cephradine
Kazi ya Cefazolin
Hutumika kwenye matibabu ya wagonjwa wa cholecystitis Hutumika kwenye matibabu ya wagonjwa wenye Maambukizi ya mfumo wa mkojo Hutumika kama kinga ya Maambukizi kabla ya upasuaji
Utofauti wa Cefazolin na dawa zingine kwenye kundi moja
Utofauti wa pekee wa dawa hii na dawa zingine za kwenye kundi hili la cephalosporin ya kwanza :
• Dawa hii hutolewa mwilini kwa njia ya mkojo kwa asilimia kubwa zaidi kuliko njia zingine. • Dawa hii nusu ya maisha ya dawa hii ni dakika 90 mpaka 150 tangu itumike mwilini
Dawa usizopaswa kutumia pamoja na Cefazolin
Dawa hii haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo; • Antithrombin alfa • Argatroban • Bivalirudin • Dalteparin • Enoxaparin • Fondaparinux • Heparin • Warfarin • Bazedoxifene • Dienogest • Estradiol • Ethinylestradiol • Probenecid
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Cefazolin
Wagonjwa wenye aleji na dawa hii au jamii ya dawa za cephalosporin
Tahadhari ya Cefazolin
Dozi yake inapaswa kupunguzwa kwa mgonjwa mwenye shida ya figo Matumizi ya muda mrefu huweza kupelekea fangasi kwenye mwili
Matumizi ya Cefazolin kwa mama mjamzito
Dawa hii ipo kwenye kundi B la usalama kwa mama mjamzito Dawa hii inaweza kutumika kwa mama mjamzito ,Tafiti za wanyama hazionyeshi hatari yeyote kwa mjamzito
Matumizi ya Cefazolin kwa mama anayenyonyesha
Inaweza kutumika kwa mama anayenyonyesha sababu hakuna madhara yeyote yaliyoripotiwa
Maudhi ya Cefazolin
Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hii ni; • Kizunguzungu • Kichefuchefu • Kutapika • Kuharisha • Homa
Endapo umesahau dozi ya Cefazolin
Je endapo utasahau dozi yako ufanyaje? Endapo ukisahau kutumia dozi yako tumia mara pale utakapokumbuka na endapo muda wa dozi nyingine umekaribia acha dozi uliyoisahau na endelea na dozi yako kama ulivyopangiwa na daktari wako
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023 16:54:56
Rejea za mada hii:-