top of page

Dawa

ULY CLINIC inakutahadharisha kuwa matumizi ya dawa pasipo ushauri wa daktari yanaweza kuleta madhara makubwa mwilini mwako.

 

Siku zote wasiliana na daktari wako kwa elimu na ushauri wa dawa gani na namna ya kutumia dawa inayoendana na hali yako halisi kama mbadala ya kujichukulia hatua mwenyewe.

Bonyeza 'Soma zaidi ' kwenye dawa unayohitaji kuanza kusoma kuhusu dawa hiyo..

Dawa Ivermectin

Dawa Ivermectin

Ivermectin ni dawa ya kuua minyoo na wadudu inayotumika kutibu magonjwa kama scabies, onchocerciasis, na minyoo ya tumbo. Hutumiwa chini ya uangalizi wa daktari, hasa kwa wajawazito, wagonjwa wa ini, na watoto wadogo.

Dawa Salbutamol

Dawa Salbutamol

Salbutamol ni dawa salama na bora kwa kutuliza dalili za matatizo ya kupumua kama pumu na bronkaitis. Inapaswa kutumika kwa tahadhari na kwa ushauri wa daktari ili kuepuka madhara yanayoweza kutokea.

Dawa Flibanserin

Dawa Flibanserin

Flibanserin (Addyi) ni dawa ya kuongeza hamu ya tendo la ndoa kwa wanawake walioko katika umri wa kuzaa wenye upungufu wa hamu ya ngono. Hufanya kazi kwa kusawazisha vichocheo vya ubongo vinavyohusiana na hisia za kingono.

Dawa Tinidazole

Dawa Tinidazole

Tinidazole ni dawa ya kupambana na vimelea aina ya protozoa na bakteria befu, hutumika kutibu magonjwa kama trichomoniasis, amoebiasis, na giardiasis. Ina nusu maisha ya saa 12–14, hivyo huchukuliwa mara moja tu kwa siku.

Insulin NPH

Insulin NPH

Insulin NPH ni insulini ya muda wa kati inayotumika kudhibiti sukari kwa wagonjwa wa kisukari aina ya 1 na 2. Inaanza kufanya kazi ndani ya saa 1-2 na athari yake hudumu kwa takriban masaa 12-16, ikisaidia kudhibiti sukari wakati wa mchana na usiku.

Insulin Lispro

Insulin Lispro

Insulin Lispro ni insulini ya haraka sana inayotumiwa kudhibiti viwango vya sukari baada ya mlo kwa wagonjwa wa kisukari aina ya 1 na 2. Hufanya kazi haraka ndani ya dakika 15 hadi 30 na athari yake hudumu kwa masaa 3-5.

Insulin glargine

Insulin glargine

Insulin glargine ni insulini ya muda mrefu inayotolewa kwa sindano mara moja kwa siku kwa ajili ya kudhibiti sukari katika damu kwa wagonjwa wa kisukari aina ya 1 na 2. Hufanya kazi polepole kwa saa 24 bila kilele, ikisaidia kuzuia mabadiliko makubwa ya sukari damu.

Medroxyprogesterone ya sindano

Medroxyprogesterone ya sindano

Medroxyprogesterone injection ni dawa ya homoni ya uzazi wa mpango inayotolewa kwa sindano kila miezi mitatu, pia hutumika kutibu hali mbalimbali za kiafya kama hedhi zisizo kawaida na saratani. Hufanya kazi kwa kuzuia ovulation na kubadilisha ukuta wa uterasi ili kuzuia ujauzito.

Kitanzi cha Levonorgestrel (Mirena)

Kitanzi cha Levonorgestrel (Mirena)

Kitanzi Levonorgestrel ni kifaa kidogo chenye homoni kinachowekwa ndani ya mji wa mimba ili kuzuia mimba kwa hadi miaka 5–8. Kina ufanisi wa zaidi ya 99% na pia husaidia kupunguza hedhi nzito na maumivu ya tumbo.

Njiti ya Etonogestrel

Njiti ya Etonogestrel

Njiti(Etonogestrel implant) ni kijiti cha uzazi wa mpango kinachowekwa chini ya ngozi na hutoa homoni kuzuia mimba kwa hadi miaka mitatu. Kifaa hiki kina ufanisi wa juu (zaidi ya 99%) na kinaweza kuondolewa wakati wowote ukihitajika.

Dawa Mifepristone

Dawa Mifepristone

Mifepristone ni dawa ya kuzuia projesteroni inayotumika kwa kutoa mimba salama na kusababisha uchungu wa uzazi. Mara nyingi hutumiwa pamoja na misoprostol kwa ufanisi wa juu.

Dawa Misoprostol

Dawa Misoprostol

Misoprostol ni dawa ya prostaglandini inayotumika kusababisha uchungu, kutoa mimba salama, na kutibu kutokwa damu baada ya kujifungua. Pia hutumika kwa vidonda vya tumbo vinavyosababishwa na NSAIDs.

Hujapata dawa unayotafuta?

 

Endapo hujapata dawa unayotafuta andika katika kiboksi kilichoandikwa  "Tafuta chochote hapa...." juu ya kurasa hii na endapo hujapata katika kiboksi hiko basi wasiliana na wafamasia wa ULY CLINIC maelezo zaidi kuhusu dawa.

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri na tiba kwa kubofya linki ya 'Mawasiliano yetu' au 'Pata tiba' chini ya tovuti hii

bottom of page