top of page

Dawa

ULY CLINIC inakutahadharisha kuwa matumizi ya dawa pasipo ushauri wa daktari yanaweza kuleta madhara makubwa mwilini mwako.

 

Siku zote wasiliana na daktari wako kwa elimu na ushauri wa dawa gani na namna ya kutumia dawa inayoendana na hali yako halisi kama mbadala ya kujichukulia hatua mwenyewe.

Bonyeza 'Soma zaidi ' kwenye dawa unayohitaji kuanza kusoma kuhusu dawa hiyo..

Dawa za wagonjwa waliofanyiwa dayalisis

Dawa za wagonjwa waliofanyiwa dayalisis

Dawa za wagonjwa waliofanyiwa dayalysis (dialysis) au wanaofanyiwa dayalisis hutumika kukabiliana na magonjwa ya figo, upungufu unaotokana na kuchujwa kwa damu n.k dawa hizi utaandikiwa na daktari wako kulingana na ushauri wa kitaalamu ambao atakupatia daktari wako. Miongoni mwa dawa wanazopatiwa wagonjwa waliofanyiwa dayalisis ni;

Dawa ya jipu ukeni

Dawa ya jipu ukeni

Jipu ukeni katika makala hii imetumika kumaanisha uvimbe maji au uvimbe wa usaha kwenye mirija ya batholin, soma zaidi kwa uelewa wa ziada kuhusu uvimbe wa batholin kwenye makala ya ‘jipu tundu la uke’ au ‘uvimbe wa batholin’.

Dawa ya kupata usingizi haraka

Dawa ya kupata usingizi haraka

Dawa za kupata usingizi haraka ni pamoja na melatonin, antihistamines, na dawa maalumu za usingizi kama benzodiazepines, zinazotumika chini ya usimamizi wa daktari. Matumizi yake hulenga kupunguza msongo wa mawazo, kutuliza mwili, na kurejesha mdundo wa usingizi, huku ikisisitizwa usalama na kuepuka utegemezi.

Dawa za fangasi wa mwili

Dawa za fangasi wa mwili

Fangasi wa mwili ni wale wanaodhuru sehemu yoyote ya mwili, hufahamika kama mashiringi na kwa jina lakitiba kama Tinea corporis.

Dawa ya kukojoa kitandani kwa watoto

Dawa ya kukojoa kitandani kwa watoto

Dawa zilizoruhusiwa na FDA/TMDA kuzuia tatizo la kukojoa kitandani kwa watoto ni dawa ya imipramine ambayo ni dawa ya kuzuia sonona na dawa inayofanya kazi kama homoni iitwayo desmopressin acetate.

Dawa ya harufu mbaya kinywani

Dawa ya harufu mbaya kinywani

Makala hii inachambua chanzo cha harufu mbaya kutoka kooni na ugumu wa kumeza, ikihusisha magonjwa ya koo, tumbo na yale ya mfumo mzima wa mwili. Inasisitiza umuhimu wa uchunguzi wa mapema na matibabu sahihi ili kuzuia matatizo makubwa zaidi.

Dawa za maumivu ya chembe ya moyo

Dawa za maumivu ya chembe ya moyo

Tiba ya maumivu ya chembe ya moyo hutegemea chanzo chake, ikiwemo dawa za kutuliza maumivu na za kupunguza asidi ya tumbo. Kwa mawe kwenye nyongo, tiba ya kudumu ni upasuaji wa kuondoa mfuko wa nyongo.

Dawa za U.T.I

Dawa za U.T.I

U.T.I inaweza kusababishwa na bakteria aina moja au zaidi na hutibiwa kwa dawa jamii ya antibayotiki yenye uwezo wa kuua kimelea aliyesababisha ugonjwa.

Dawa za maambukizi ya Human papillomavirus (HPV)

Dawa za maambukizi ya Human papillomavirus (HPV)

Maambukizi ya kirusi cha HPV huwa hayatibiki, madhara yanayoletwa na kirusi huyu huwa yanatibika pamoja. Hata hivyo kuna chanjo ya kinga pia ya kuzuia kupata maambukizi ya kirusi cha HPV inayotolewa kwa wanawake ambao bado hawajaanza kushiriki ngono au wasio na maambukizi ya kirusi huyu.

Dawa za kuyeyusha damu

Dawa za kuyeyusha damu

Dawa za kuyeyusha damu hujumuisha dawa za kufanya damu iwe nyepesi, kuyeyusha bonge la damu lililoganda au zile za kuzuia chembe sahani za damu kukusanyika ili kutengeneza bonge la damu.

Dawa za  kolestro

Dawa za kolestro

Dawa za kolestro katika makala hii imetumika kumaanisha dawa za kupunguza kiwango cha kolestro (lehemu) kwenye damu na hufahamika kwa jina jingine kama dawa jamii ya statin au dawa za kushusha lehemu wkenye damu.

Dawa ya kutibu Vajinosis ya bakteria

Dawa ya kutibu Vajinosis ya bakteria

Vaginosis ya bakteria ni ugonjwa wa vajinosis ya bakteria ni hali inayoletwa na ongezeko kubwa la bakteria waishio ndani ya uke hivyo kuwazidi bakteria walinzi ambao pia huishi ndani ya uke

Hujapata dawa unayotafuta?

 

Endapo hujapata dawa unayotafuta andika katika kiboksi kilichoandikwa  "Tafuta chochote hapa...." juu ya kurasa hii na endapo hujapata katika kiboksi hiko basi wasiliana na wafamasia wa ULY CLINIC maelezo zaidi kuhusu dawa.

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri na tiba kwa kubofya linki ya 'Mawasiliano yetu' au 'Pata tiba' chini ya tovuti hii

bottom of page