top of page
Elimu ya magonjwa kwa mjamzito
Sehemu hii utajifunza maelezo ya ziada kuhusu matatizo mbalimbali ya kiafya wakati wa ujauzito. Unashauriwa siku zote kuwasilaina na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile iliyoandikwa humu ili kupata ushauri unaoendana na hali yako ya kiafya.

Dalili za mimba ya miezi saba
Ukuaji wa mtoto katika miezi saba huendelea kwa kasi, hivyo kufuatilia mijongeo ya mtoto kila siku, kudhibiti magonjwa yaliyopo, kula lishe bora na kutambua mapema dalili za hatari ni hatua muhimu zinazochangia ujauzito salama. Kumbuka kuwa si kila dalili mpya ni ya kawaida; mabadiliko kama kupungua kwa mijongeo ya mtoto, kutoka damu au maji ukeni, maumivu makali ya tumbo au kichwa yanahitaji uchunguzi wa haraka katika kituo cha afya.
bottom of page




