top of page

Magonjwa na saratani mbalimbali

Sehemu hii utasoma kuhusu hali na magonjwa mbalimbali

Matege

Matege

Matege husababishwa na hali ya mifupa kuwa laini na dhaifu, hali hii husababishwa na kuwepo kwa upungufu endelevu wa madini ya vitamini D kwa watoto.

Furunkulosisi (furunculosis)

Furunkulosisi (furunculosis)

Furunkulosisi (furunculosis) ni hali ya kupata majipu yanayojirudia mara kwa mara. Jipu ni maambukizi ya kina ya kinyweleo, mara nyingi kwa bakteria Staphylococcus aureus, linaloleta uvimbe mwekundu wenye maumivu na usaha. Huhusiana na kubeba bakteria hao puani, kisukari na usafi. Majipu makubwa hutolewa usaha; yanayojirudia yanahitaji kuondoa bakteria mwilini.

Vipele vya Fordyce (Fordyce spots)

Vipele vya Fordyce (Fordyce spots)

Vipele vya Fordyce (Fordyce spots) ni vipele vidogo vya rangi ya njano au nyeupe, vya ukubwa wa milimita 1–3, vinavyoonekana kwenye mpini au kichwa cha uume, pumbu, mashavu ya uke au midomo. Ni tezi za kawaida za mafuta zilizo karibu na uso wa ngozi. Si ugonjwa wa zinaa, haviambukizi wala si saratani, na kwa kawaida havihitaji matibabu.

Salmonellosisi (salmonellosis)

Salmonellosisi (salmonellosis)

Salmonellosisi (salmonellosis) ni maambukizi ya bakteria wa Salmonella wasio wa taifodi, wanaopatikana kwenye kuku, mayai, nyama na maziwa yasiyoiva au yasiyochemshwa. Huleta kuharisha, maumivu ya tumbo, homa na kutapika saa 6–72 baada ya kula. Wengi hupona ndani ya wiki moja kwa maji na ORS; antibiotiki hutolewa kwa makundi hatarishi tu.

bottom of page