Magonjwa na saratani mbalimbali
Sehemu hii utasoma kuhusu hali na magonjwa mbalimbali

Kiharusi (stroke)
Kiharusi (stroke) hutokea damu inaposhindwa kufika sehemu ya ubongo kwa sababu mshipa umeziba au umepasuka. Dalili huja ghafla: uso kupinda, mkono au mguu kulegea upande mmoja, kushindwa kuongea. Ni dharura – kila dakika ina thamani. Shinikizo la juu la damu ndicho chanzo kikuu kinachoweza kudhibitiwa.

Sisti kwenye ovari (ovarian cyst)
Sisti kwenye ovari (ovarian cyst) ni kifuko chenye majimaji au tishu kwenye ovari. Nyingi ni za kawaida zinazotokana na mzunguko wa hedhi, hazina madhara na hupotea zenyewe ndani ya miezi 2–3. Chache huwa kubwa, hujisokota au kupasuka na kuleta maumivu makali. Ultrasound huamua kama ifuatiliwe au iondolewe.

Kuvunjika kwa uume (penile fracture)
Kuvunjika kwa uume (penile fracture) ni kupasuka kwa utando mgumu unaozunguka mirija ya kusimamisha uume, wakati uume umesimama – mara nyingi wakati wa kujamiiana kwa nguvu. Huleta mlio wa kupasuka, maumivu ya ghafla, uume kulala haraka na kuvimba kama biringanya. Ni dharura ya upasuaji – kuwahi huzuia upungufu wa nguvu za kiume.

Fangasi ukeni (vaginal candidiasis)
Fangasi ukeni (vaginal candidiasis) ni maambukizi ya fangasi jamii ya Candida yanayoleta muwasho mkali, uchafu mweupe mzito kama maziwa mgando na kuungua sehemu za siri. Si ugonjwa wa zinaa. Huchochewa na antibiotiki, ujauzito, kisukari na kinga kushuka, na hutibika kwa dawa za kuweka ukeni au za kumeza.
