top of page

Magonjwa na saratani mbalimbali

Sehemu hii utasoma kuhusu hali na magonjwa mbalimbali

Ugumba (infertility)

Ugumba (infertility)

Ugumba (infertility) ni kushindwa kupata mimba baada ya miezi 12 ya kujamiiana mara kwa mara bila kinga (miezi 6 kwa mwanamke zaidi ya miaka 35). Huwapata takribani mtu 1 kati ya 6. Chanzo kinaweza kuwa kwa mwanamke, mwanaume au wote – kwa hiyo wenzi wote wawili wachunguzwe. Matibabu mengi yapo.

Bawasiri (haemorrhoids)

Bawasiri (haemorrhoids)

Bawasiri (haemorrhoids) ni mishipa ya damu iliyovimba ndani au nje ya tundu la haja kubwa. Huleta damu nyekundu baada ya kujisaidia, kinyama kutoka nje, muwasho au maumivu. Chanzo kikuu ni kukenya kwa sababu ya choo kigumu. Hutibiwa kwa lishe yenye nyuzinyuzi na maji, dawa za kupaka, na kwa bawasiri kubwa, upasuaji mdogo.

Mafua makali ya influenza (flu)

Mafua makali ya influenza (flu)

Mafua makali ya influenza (flu) ni ugonjwa wa virusi vya influenza unaoanza ghafla kwa homa kali, maumivu ya mwili, kikohozi na uchovu mkubwa. Wengi hupona ndani ya wiki moja, lakini wazee, wajawazito, watoto wadogo na wenye magonjwa sugu huweza kupata nimonia. Chanjo ya kila mwaka ndiyo kinga bora.

Saratani ya tezi dume (prostate cancer)

Saratani ya tezi dume (prostate cancer)

Saratani ya tezi dume (prostate cancer) ndiyo saratani inayotokea zaidi kwa wanaume Tanzania, hasa baada ya miaka 50. Mwanzoni haina dalili; baadaye huleta shida ya kukojoa na maumivu ya mifupa ikisambaa. Wanaume weusi hupata mapema na kwa ukali zaidi. Ikigunduliwa mapema kwa PSA na uchunguzi, hutibika vizuri.

bottom of page