Sehemu ya Matangazo
ULY CLINIC haiidhinishi au kupendekeza kampuni au bidhaa zinazotangazwa. Mapato yanayotokana na matangazo husaidia kuunga mkono dhamira yetu ya kutoa huduma kwa jamii bila kutafuta faida.
Sehemu hii utasoma kuhusu hali na magonjwa mbalimbali
Saratani ya damu (leukemia)
Saratani ya damu (leukemia) ni saratani ya uboho ambapo chembe nyeupe zisizo za kawaida huzaliana kupita kiasi na kuzuia utengenezaji wa damu ya kawaida. Huleta upungufu wa damu, maambukizi ya mara kwa mara na kutokwa damu kirahisi; nyingi hutibika zikigunduliwa mapema.
Kisonono (gono, gonorrhoea) ni ugonjwa wa zinaa wa bakteria unaoleta usaha na maumivu ya kukojoa kwa wanaume, lakini mara nyingi hauna dalili kwa wanawake. Hutibika kwa dawa sahihi kutoka kituo cha afya; usipotibiwa huleta ugumba na maambukizi ya via vya uzazi.
Kiharusi cha mpito (TIA) ni shambulio la muda mfupi la dalili za kiharusi linalopotea lenyewe ndani ya dakika au saa chache. Ni onyo la hatari: bila uchunguzi na kinga ya haraka, kiharusi kikubwa huweza kufuata ndani ya siku chache.
Malaria ni ugonjwa unaosababishwa na vimelea vya Plasmodium vinavyoenezwa na mbu jike aina ya Anopheles. Huleta homa, kutetemeka na maumivu ya mwili; malaria kali huua haraka hasa watoto na wajawazito. Pima kwanza – malaria hutibika kabisa kwa dawa sahihi.