top of page

Vidokezo vya Afya

Maji na mafuta ni miongoni mwa tiba ya kupasuka midomo

Maji na mafuta ni miongoni mwa tiba ya kupasuka midomo

Kupasuka midomo ni tatizo linalowapata watu wengi kwa nyakati mbalimbali ndani ya mwaka. Visababishi vinaweza kuwa hali ya hewa ya baridi au yenye ukavu, kuungua na mwanga wa jua, kupulizwa na upepo mkali, kulamba midomo na kupumua kupitia mdomo. Kunywa maji ya kutosha, paka mafuta au 'lip balm' na kujifunika midomo huwa ni tiba pia kinga.

Maji ya bamia huchochea uponyaji wa vidonda vya tumbo

Maji ya bamia huchochea uponyaji wa vidonda vya tumbo

Ukuta wa ndani ya tumbo kwa kawaida umefunikwa kwa ute ute wa mlenda unaozuia kuta za chini zisiunguzwe na tindikali zinazozalishwa tumboni. Kwa mtu mwenye vidonda vya tumbo, ute huu huwa dhaifu na udhaifu husambaa eneo kubwa zaidi. Matumizi ya maji ya bamia hurejesha kuta hii na kuharakisha uponyaji utokee.

Maji ya mwanamke aliyekojozwa

Maji ya mwanamke aliyekojozwa

Maji yanyotoka kwa mwanamke aliyekojozwa huwa mweupe kama maziwa, mtamu, usio na harufu ya mkojo na ujazo wa kijiko kimoja cha chai. Maji yasiyofanana na hayo si maji ya kukojozwa bali ni mkojo wa kawaida tu.

Majibu 7 ya kipimo cha HIV 1/2 SD bioline 3.0

Majibu 7 ya kipimo cha HIV 1/2 SD bioline 3.0

Kipimo cha SD bioline huweza kutoa aina 7 za majibu yanayopaswa kutafsiriwa kwa usahihi. Kufahamu aina hizo kabla ya kufanya kipimo huepusha gharama na athari zinazoweza kutokea kwa mpimaji na anayejipima mwenyewe.

Majibu chanya ya VVU pasipo VVU

Majibu chanya ya VVU pasipo VVU

Majibu chanya ya kipimo cha HIV SD bioline licha ya kushuku maambukizi ya VVU, huweza kuwa chanya kwa mwenye kaswende, kichocho, minyoo, shambulio binafsi la kinga, ujauzito n.k. Majibu chanya yanapaswa kuthibitishwa kwa kipimo cha HIV Uni-Gold au vingine vyenye ufanisi zaidi.

bottom of page