top of page

Vidokezo vya Afya

Aina za PEP zinazotumika

Aina za PEP zinazotumika

Dawa za PEP zinazotumika huwa na mchanganyiko wa dawa ambao ni tenofovir na emtricitabine na raltegravir au na dolutegravir au na darunavir na ritonavir.

Alfajiri ni muda mzuri wa kushiriki ngono

Alfajiri ni muda mzuri wa kushiriki ngono

Tafiti zinaonyesha kuwa, kiwango cha homoni testosterone inayokupa nguvu za kiume huongezeka kwa kiasi kikubwa kati ya sa moja hadi sa tatu asubuhi. Ongezeko la testosterone alfajiri huwafanya wanaume wengi wawe na nguvu zaidi na kuchelewa kumaliza wanaposhiriki ngono asubuhi. Hii ni kweli kwa wanaume chini ya umri wa miaka 46

Baadhi ya dawa zilizoisha muda wa matumizi zinaweza kutumika kwa tahadhari

Baadhi ya dawa zilizoisha muda wa matumizi zinaweza kutumika kwa tahadhari

Tafiti nyingi zinaonyesha, kiini cha dawa hupungua tangu siku dawa inatengenezwa na asilimia 90 ya kiini cha dawa nyingi, hubakia kwenye dawa hadi miaka mitano tangu siku ya kuisha muda wa matumizi. Endapo unahitaji matokeo ya asilimia 100 kutoka kwenye dawa, tumia dawa ambayo haijaisha muda wake wa matumizi.

Chai ya kitunguu swaumu na tangawizi

Chai ya kitunguu swaumu na tangawizi

Mbali na kuongeza kinga ya mwili, kuondoa sumu mwilini, kuzuia saratani, kudhibiti sukari na shinikizo la damu na kushusha kiwango cha lehemu kwenye damu, chai ya kitunguu swaumu na tangawizi humwezesha mwanaume kufanya ngono kwa muda mrefu zaidi. Tumia mazao haya kila siku kwa afya yako.

Chai ya ndizi mbivu

Chai ya ndizi mbivu

Kwa kula ndizi mbivu utapata virutubisho kama vitamin B6, potassium, magnesium, manganese na shaba. Hata hivyo chai ya ndizi mbivu na maganda yake huwa na vitamin B6, potassium na tryptophan kwa wingi kiasi cha kuweza kukupa usingizi, kuthibiti shinikizo la damu na kuondoa sumu mwilini.

bottom of page