top of page

Vidokezo vya Afya

Matumizi ya vidonge vya majira

Matumizi ya vidonge vya majira

Vidonge vya majira au uzazi wa mpango, vimetengenezwa kwa homon zinazozuia ujauzito kwa kusimamisha uzalishaji wa yai na manii kuingia ndani ya mfuko wa kizazi. Unaweza anza vidonge vya majira siku ya kwanza ya hedhi au siku yoyote kama huna ujauzito na upo tayari kutumia njia nyongeza siku saba za mwanzoni.

Matumizi ya vilevi kwa mama mjamzito| ULY CLINIC

Matumizi ya vilevi kwa mama mjamzito| ULY CLINIC

Matumizi ya pombe na madawa ya kulevya kwa mama ni hatari kwa afya ya mama na ya mtoto. Epuka pombe na madawa ya kulevya kwa afya bora.

Maudhi ya PEP

Maudhi ya PEP

Kichefuchefu, mvurugiko wa tumbo, maumivu ya kichwa, kizunguzungu, uchovu mkali na kuhara ni baadhi ya maudhi madogo ya kutumia PEP ambayo huisha kwa jinsi muda unavyokwenda.

Maudhi ya kuacha vidonge vya majira

Maudhi ya kuacha vidonge vya majira

Mtumiaji wa muda mrefu wa njia za uzazi wa mpango zenye vichocheo anapoacha huweza patwa na hedhi nzito, yenye maumivu makali au isiyoeleweka, chunusi, kuota nywele zisizotakiwa, kutopata ujauzito kwa wakati n.k. Wasiliana na daktari kama dalili zitadumu zaidi ya miezi sita.

Maumivu ya fantomu

Maumivu ya fantomu

Fantomu ni hisia ya maumivu kutoka kwenye kiungo cha mkono au mguu kilichotengwa na mwili kwa upasuaji baada ya kuharibiwa na ugonjwa au ajali. Hutokea sana kwa wagonjwa waliokuwa na maumivu makali kabla ya upasuaji, tiba yake hutofautiana baina ya mtu na mtu na huhusisha matumizi ya dawa mbalimbali kabla ya kufahamu ipi inayofaa zaidi.

bottom of page