top of page

Vidokezo vya Afya

Ngozi ya chungwa

Ngozi ya chungwa

Ushawishi wa homoni za kike na ukusanyaji wa sumu na uchafu hususani maeneo ya makalio na mapaja husababisha ngozi kutunza mafuta na maji na hivyo kuifanya iwe na mwonekano wa ganda la chungwa. Matumizi ya sharubati ya tango, nanasi na figili hudhibiti na kuondoa tatizo hili.

Nguvu za kiume

Nguvu za kiume

Upungufu wa Nguvu za kiume huelezewa kama kukosa uwezo wa kudumisha uume kusimama katika muda unaotosheleza mahitaji ya kujamiiana. Tatizo hili linaweza kusababishwa na madhaifu mbalimbali au matatizo ya akili.

Nini kinafuata baada ya kuanza PEP?

Nini kinafuata baada ya kuanza PEP?

Utafanyiwa tena kipimo cha kuangalia maambukizi ya VVU kwenye damu baada ya wiki 4 yaani wiki ya 6 na 12.

Njia nzuri ya kuongeza damu

Njia nzuri ya kuongeza damu

Hutegemea kiwango cha upungufu wa damu mwilini na huweza kuhusisha tiba lishe, dawa au kuongezwa damu.

Njia za dawa kuingia mwilini

Njia za dawa kuingia mwilini

Ili kufanikiwa kwa tiba, unapaswa kutumia dawa kwa njia sahihi uliyoelekezwa na daktari au mtoa dawa. Kwa ufanisi wa dawa, tumia kama ulivyoelekezwa na daktari wako.

bottom of page