top of page

Vidokezo vya Afya

Punguza kupigwa na mionzi ya simu isiyo ya lazima kwa usalama wa afya yako

Punguza kupigwa na mionzi ya simu isiyo ya lazima kwa usalama wa afya yako

Usiongee nayo kwa muda mrefu au wakati wa kuchaji, kulala karibu, kuhifadhi maeneo ya kifuani au kuweka karibu na sehemu za siri simu yako ya mkononi. Ukifanya hivi utaepuka kupigwa na mionzi isiyoya lazima inayozalishwa na simu yako. Fanya hivi kujilinda na hatari ya kupata saratani

Salmonella typhi husababisha taifod

Salmonella typhi husababisha taifod

Salmonella typhi ni kimelea pekee anayesababisha taifodi kali kwa binadamu, kimelea huyu huweza fanya makazi na kuzaliana kwenye kibofu cha nyongo kwa muda mrefu hivyo kusababisha taifodi sugu. Endapo taifodi yako haiishi kwa matibabu, inawezekana una vimelea hao kwenye kibofu cha nyongo. Ukipata matibabu sahihi utapona na kuwakinga ndugu kupata maambukizi.

Sharubati ya Kutibu U.T.I

Sharubati ya Kutibu U.T.I

Sharubati ya beri ya bluu pamoja na tui la nazi hutibu na kupunguza hatari ya kupata maambukizi ya U.T.I kwa kuua na kudhoofisha uwezo wa bakteria wanaosababisha U.T.I kuingia kwenye mfumo wa mkojo.

Shinikizo la juu la damu ni muuaji wa siri

Shinikizo la juu la damu ni muuaji wa siri

Shinikizo la juu la damu, watu wengi hufahamu kama presha, ni tatizo linaloua kwa siri watu zaidi ya milioni saba kila mwaka duniani. Hii ni kwa sababu tatizo hili huwa halionyeshi dalili yoyote ile linapotokea. Weka mikakati ya kujikinga, anza kwa kupima kila baada ya miezi miwili.

Soma tarehe ya mwisho wa matumizi kwa kila dawa unayonunua

Soma tarehe ya mwisho wa matumizi kwa kila dawa unayonunua

Kufahamu tarehe ya mwisho wa matumizi ya dawa ni njia mojawapo ya kuzuia madhara yanayoweza kujitokeza pamoja na usugu wa vimelea vya maradhi dhidi ya dawa hiyo. Jenga tabia ya kusoma mwisho wa matumizi wa kila dawa unayonunua.

bottom of page