top of page
Vidokezo vya Afya

Dawa na virutubisho vinavyotibu COVID-19
Tafiti zinaonyesha, dawa azithromycin, madini ya zinc, vitamini C na D na dexamethasone huwa na uwezo wa kukukinga na kutibu magonjwa ya mfumo wa upumuaji kama COVID-19 . Unashauriwa kupata vitamini C na D na madini ya zinc kutoka kwenye vyakula, endapo unahitaji dawa wasiliana na daktari wako.

Epuka kula chumvi nyingi
Kula chumvi nyingi kila siku huongeza hatari ya kupata shinikizo la juu la damu na kiharusi, hivyo ni muhimu kujihadhari kwa kupunguza chumvi kwenye chakula pamoja na kuepuka vyakula vya kukaangwa na vyakula vilivyosindikwa kama vibanzi na soseji. Badala ya kuongeza chumvi, tumia viungo vya asili kama limao, kitunguu saumu, tangawizi au majani ya chai ili kuboresha ladha ya chakula bila kuongeza hatari kiafya.
bottom of page



