top of page
Vidokezo vya Afya

Fungua dirisha wakati unasafiri
Vimelea vya maradhi ya mfumo wa upumuaji kama kifua kikuu, mafua, COVID 19 n.k huambukizwa kwa njia ya hewa wakati unasafiri na watu wengi. Mgonjwa akipiga chafya, akikohoa au kucheka hutoa vimelea wanaokaa kwenye hewa kwa masaa kadhaa. Epuka maambukizi haya wakati wa safari kwa kufungua dirisha au kuwasha kiyoyozi wakati wote ili kutoa hewa chafu nje.

Ganzi na maumivu ya mikono wakati wa ujauzito
Ganzi na hisia za maumivu ya mikono wakati wa ujauzito husababishwa na mgandamizo kwenye mshipa wa fahamu unaopita shimo la kapo. Kukanda kwa maji baridi kisha moto, kufanya zoezi la kukunja ngumi na kunyoosha vidole au kukunja na kunyoosha maungio ya kiganja ni tiba asili ya maumivu hayo.
bottom of page



