Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:
Dkt. Mangwella S, MD
Dkt. Salome A, MD
2 Aprili 2026, 16:17:51

Kipindi cha pili cha Ujauzito
Huanzia wiki ya 13 hadi 27 ya ujauzito. Kipindi hiki huwa ni katikati ya safari ya ujauzito, kijusi hukua kutoka urefu wa sentimita 7.5 hadi 23 na kuongezeka uzito kutoka gramu 30 hadi 820. Dalili za kichefuchefu na kutapika huwa tayari zimepungua sana na mtoto huwa si mkubwa kiasi cha kukufanya ujihisi vibaya mwilini.

Nini hutokea mwilini?
Katika kipindi cha pili cha ujauzito unaweza kupata dalili na mabadiliko yafuatayo mwilini mwako.
Kukua kwa tumbo na matiti.
Jinsi kizazi kinavyozidi kuongezeka ili kuongeza nafasi ya kijusi kinachokua ndani, nje ya mwili utaonekana tumbo linaongezeka. Matiti yako pia yatakuwa yakiongezeka taratibu na hivyo utahitaji sidiria ya kuyabeba vema.
Uchungu wa uongo
Uchungu wa uongo ni hisia za uchungu kiasi, usioeleweka mpangilio na huwa mithiri ya kubana kwa misuli ya tumbo la uzazi. Hutokea sana wakati wa mchana au jioni, baada ya kufanya ngono au kazi ya kimwili. Unashauriwa kuwasiliana na daktari wako kama maumivu yakiwa yanatokea kwa mpangilio unaoeleweka na kuongezeka kwa makali jinsi muda unavyoenda maana inaweza kuwa ishara ya uchungu kabla ya wakati.
Mabadiliko ya ngozi
Mabadiliko ya homoni wakati wa ujauzito huchochea ongezeko la pigmenti melanini inayoipa rangi ngozi. Hii hupelekea kutokea kwa mstari mweusi chini ya kitovu na mabaka meusi usoni. Mabadiliko haya hutokea sana na mara nyingi hupotea baada ya kujifungua.
Kupigwa na mwanga wa jua kunaweza kuongeza mabadiliko ya ngozi, unaweza kupata michirizi mieusi, brauni, au zambarau tumboni, kwenye matiti, matakoni au mapajani. Â Alama za kuvutika kwa ngozi zinaweza kutozuilika hata hivyo hupungua baada ya kujifungua.
Matitizo ya pua
Wakati wa ujauzito kiwango cha homoni huongezeka na mwili hutengeneza damu nyingi. Hii husababisha kuta laini za pua kuvimba na kutoka damu kirahisi na kusababisha kuta hizo kuvimba na damu kutoka. Maji ya chumvi huweza saidia kupunguza kuvimba. Kunywa maji ya kutosha na matumizi ya kiongeza unyevu kwenye hewa na mafuta ya yenye petroleum husaudia kulainisha kuta za pua.
Matatizo ya meno
Kutokana na mabadiliko ya homoni na kiungulia, fizi kuwa na hisia zaidi kwenye dawa na mswaki pamoja na kutokwa damu.
Mabadiliko na dalili zingine zinazotokea kipindi cha pili cha ujauzito
Kizunguzungu
Miguu kubana
Kutokwa na ute ukeni wenye rangi ya maji au maziwa usio na harufu wala maumivu
Maambukizi ya njia ya mkojo
Kuhisi umechoka
Ujauzito katika wiki
Ili kufahamu dalili na ukuaji wa hatua kwa hatua bofya makala halisi katika wiki hiyo
Soma kuhusu ujauzito kwa miezi
Mambo ya kuzingatia kwenye kipindi cha pili cha ujauzito
Katika kipindi cha pili cha ujauzito, unapaswa kuendelea kuhudhuria kliniki ya ujauzito ili kusaidia kugundua matatizo yoyote kwako na kwa mtotot tumboni. Utapimwa uzito, shinikizo la damu, kimo cha mimba na vingine ambavyo ni muhimu kulingana na mahali ulipo.
Hakikisha unaripoti dalili zozote za hatari au zile ambazo ungependa upate ufafanuzi kwa mtaalamu wa afya wakati huu wa kuhudhuria kliniki.
Majina mengine ya makala hii
Miezi mitatu ya pili ya ujauzito
Traimista ya pili
Miezi minne hadi sia ya ujauzito
Vipindi vingine vya ujauzito
Somo pia kuhusu vipindi vingine vya ujauzito kwa kubofya linki zifuatazo
Imeandikwa:
2 Aprili 2026, 16:17:51
ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.
​
Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.
Rejea za mada hii:
