top of page

Mwandishi:

Mhariri:

Imeboreshwa:

ULY CLINIC

ULY CLINIC

31 Oktoba 2026, 15:23:37

Maumivu ya viungo husababishwa na nini?

Jibu kwa ufupi


Jibu kwa ufupi: Pumzika, barafu au joto, paracetamol, punguza uzito. Kiungo kimoja cha moto, kilichovimba na homa – hospitali leo. Soma Gauti.


Maelezo


Visababishi


  • Majeraha, matumizi kupita kiasi.

  • Osteoarthritis – maumivu yanayoongezeka kwa matumizi, magoti/nyonga.

  • Gauti – kiungo kimoja ghafla, kidole gumba cha mguu.

  • Baridi yabisi (RA) – viungo vidogo vya mikono pande zote mbili, kukakamaa asubuhi zaidi ya saa 1; soma Baridi yabisi.

  • Virusi – chikungunya, dengue (soma Dengue), hepatitis B, VVU.

  • Selimundu – maumivu makali ya ghafla; soma Selimundu.

  • Homa ya baridi yabisi ya moyo – watoto/vijana baada ya koo kuuma; viungo vikubwa kuhama.

  • Gono ya viungo, TB ya viungo.

  • Lupus, psoriasis – magonjwa ya kinga.


Vipimo


  • Damu kamili, ESR/CRP, uric acid, RF, VVU.

  • X-ray.

  • Kutoa maji ya kiungo kwa kiungo kimoja kilichovimba.


Nini cha kufanya


  • Pumzika kiungo kilichoumia; barafu siku 2 za mwanzo.

  • Mazoezi ya kuimarisha misuli kwa maumivu ya muda mrefu.

  • Punguza uzito – hupunguza maumivu ya magoti.

  • Paracetamol; NSAIDs kwa muda mfupi tu.

  • Usichome sindano za steroid mara kwa mara bila ushauri.


Dalili za hatari


Hospitali mara moja ukiwa na:


  • Kiungo kimoja cha moto, chekundu, kilichovimba na homa.

  • Mtoto mwenye maumivu ya viungo, homa na kupumua kwa shida au moyo kwenda kasi.

  • Maumivu makali kwa mwenye selimundu.


Lini umwone daktari


  • Maumivu zaidi ya wiki 2.

  • Viungo vingi kuvimba na kukakamaa asubuhi.

  • Kupungua uzito, homa ya muda mrefu.

  • Upele pamoja na maumivu ya viungo.


Maswali yanayoulizwa mara kwa mara


1. Maumivu ya viungo husababishwa na nini?

Majeraha, kuchakaa, gauti, baridi yabisi, virusi na mengine.

2. Chikungunya huleta maumivu ya viungo?

Ndiyo, huweza kudumu wiki hadi miezi.

3. Kiungo kimoja cha moto na homa?

Dharura – hospitali leo.

4. Uzito unachangia?

Ndiyo, hasa magoti.

5. Dawa gani ya maumivu?

Paracetamol; NSAIDs kwa muda mfupi.

6. Nipime nini?

Damu, uric acid, RF, na X-ray kulingana na dalili.

Imeandikwa:

2 Aprili 2026, 17:07:10

ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.

​

Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.

Rejea za mada hii:

  1. National Institute for Health and Care Excellence. Osteoarthritis in over 16s: diagnosis and management (NG226). London: NICE; 2022.

  2. Aletaha D, Smolen JS. Diagnosis and management of rheumatoid arthritis: a review. JAMA. 2018;320(13):1360–72.

  3. World Health Organization. Chikungunya fact sheet. Geneva: WHO; 2025.

  4. Ministry of Health, United Republic of Tanzania. Standard Treatment Guidelines and National Essential Medicines List (STG/NEMLIT), 7th edition. Dodoma: Ministry of Health; 2026.

bottom of page