top of page

Afya ya Mtoto

Kusimama kwa mtoto

Kusimama kwa mtoto

Watoto wanaweza kuanza kusimama kwa kushikilia kitu kuanzia karibu miezi 5–11, na kusimama bila msaada kunaweza kuanza takribani miezi 7–17; hivyo tofauti ya muda kati ya watoto inaweza kuwa kubwa. Mtoto ambaye hajaanza kusimama bila msaada kufikia karibu miezi 17 anapaswa kutathminiwa, na mzazi anapaswa kutafuta ushauri mapema zaidi ikiwa kuna udhaifu, kutumia upande mmoja zaidi au kupoteza uwezo aliokuwa nao.

Kupumua kwa shida kwa mtoto

Kupumua kwa shida kwa Mtoto

Kunaweza kusababishwa na mafua, nimonia, pumu, mzio, kitu kuziba njia ya hewa au magonjwa ya moyo na mapafu, hivyo chanzo kinapaswa kutambuliwa. Mtoto anayepumua kwa shida, kuvuta kifua ndani, kushindwa kunyonya au kunywa, kubadilika rangi au kulegea anahitaji huduma ya haraka ili kuzuia madhara makubwa.

Dalili za upungufu wa maji mwilini kwa watoto

Upungufu wa maji mwilini kwa watoto

Hutokea mtoto anapopoteza maji na chumvi nyingi kuliko anavyoweza kurejesha, mara nyingi kutokana na kuhara, kutapika au homa; dalili zake ni pamoja na kiu, midomo na ulimi kukauka, macho kudidimia, kupungua kwa mkojo, kulia bila machozi, ngozi kuwa kavu na mtoto kuwa dhaifu au mnyonge. Kutambua dalili mapema, kumpa ORS na kuendelea kunyonyesha husaidia kuzuia hali kuwa mbaya. Mtoto anayeshindwa kunywa au kunyonya, kutokojoa, kutapika kila kitu, kuwa mlegevu sana au kupoteza fahamu anahitaji huduma ya haraka.

Utosi wa Mtoto

Utosi wa mtoto (Fontaneli)

Ni sehemu ya kawaida ya ukuaji wa fuvu inayoruhusu ubongo kukua na husaidia kichwa kupita vema wakati wa kuzaliwa. Mara nyingi utosi wa mbele hufunga kati ya miezi 12 hadi 18, lakini tofauti ndogo zinaweza kutokea bila kumaanisha tatizo. Mabadiliko kama utosi kuzama sana, kuvimba na kuwa mgumu, kuchelewa au kufunga mapema pamoja na dalili kama homa, degedege, kutapika au mabadiliko ya ukuaji yanahitaji uchunguzi wa mtaalamu wa afya.

Henia ya kitovu kwa watoto

Henia(ngiri) ya Kitovu kwa Watoto

Ni uvimbe unaotokea pale sehemu ya ndani ya tumbo inapopita kwenye eneo dhaifu la kitovu, na kwa watoto wengi hupona yenyewe bila upasuaji kadiri misuli ya tumbo inavyokua. Wazazi wanapaswa kuepuka kufunga vitu kwenye kitovu na kufuatilia dalili za hatari kama maumivu, uvimbe mgumu, kutapika au mabadiliko ya rangi ya kitovu ili kupata matibabu kwa wakati.

Kutapika na Kichefuchefu kwa Mtoto mdogo

Kutapika na Kichefuchefu kwa Mtoto mdogo

Kutapika au kuonyesha kama mtoto anataka kutapika kila siku kunaweza kusababishwa na kucheua, ulaji usiofaa au matatizo mengine ya mfumo wa chakula. Ni muhimu kufuatilia ukuaji na dalili hatari, na mtoto apimwe na mtaalamu wa afya ikiwa hali inaendelea, mtoto haongezeki uzito au ana dalili za hatari.

bottom of page