top of page

Dawa

ULY CLINIC inakutahadharisha kuwa matumizi ya dawa pasipo ushauri wa daktari yanaweza kuleta madhara makubwa mwilini mwako.

 

Siku zote wasiliana na daktari wako kwa elimu na ushauri wa dawa gani na namna ya kutumia dawa inayoendana na hali yako halisi kama mbadala ya kujichukulia hatua mwenyewe.

​

Bonyeza 'Soma zaidi ' kwenye dawa unayohitaji kuanza kusoma kuhusu dawa hiyo..

Dawa Ambroxol

Dawa Ambroxol

Ambroxol ni dawa ya kuyeyusha makohozi inayosaidia kupunguza mnato wa ute kwenye njia ya hewa na kurahisisha kukohoa na kupumua. Hutumika sana katika magonjwa ya mfumo wa upumuaji kama bronchitis, COPD na kikohozi chenye makohozi mazito.

Dawa Bromhexine

Dawa Bromhexine

Bromhexine ni dawa ya kuyeyusha makohozi (mucolytic) inayosaidia kupunguza mnato wa makohozi na kurahisisha utolewaji wake kwenye magonjwa ya njia ya hewa.
Hutumiwa sana katika bronchitis, pumu yenye makohozi na COPD ili kuboresha upumuaji.

Dawa ya Dextromethorphan

Dawa ya Dextromethorphan

Dextromethorphan ni dawa ya kuzuia kikohozi kikavu inayofanya kazi kwenye mfumo wa kati wa fahamu(Ubongo) kwa kupunguza msisimko wa kituo cha kikohozi bila kutibu chanzo cha ugonjwa. Hutumika kwa kikohozi cha muda mfupi, inapaswa kutumiwa kwa tahadhari kwa watoto, wajawazito, na kuepukwa pamoja na pombe au dawa zinazoongeza hatari ya madhara ya mfumo wa fahamu.

Dawa Chlorpheniramine

Dawa Chlorpheniramine

Chlorpheniramine ni dawa ya antihistamine inayotumika kupunguza dalili za mzio kama mafua ya mzio, chafya, kuwashwa na kikohozi kinachosababishwa na mzio. Hufanya kazi kwa kuzuia histamine mwilini lakini inaweza kusababisha kusinzia, hivyo inapaswa kutumiwa kwa tahadhari, hasa kwa wazee, wajawazito na wanaonyonyesha.

Dawa Theophylline

Dawa Theophylline

Theophylline ni bronchodilator inayotumika kudhibiti pumu, COPD, na kuziba kwa njia za bronkai, lakini inaweza kusababisha mapigo ya moyo kwenda kasi, degedege, na kizunguzungu. Dozi lazima ichaguliwe na daktari kwa kuzingatia umri, uzito, magonjwa mengine, na dawa zinazoshirikiana.

Hujapata dawa unayotafuta?

 

Endapo hujapata dawa unayotafuta andika katika kiboksi kilichoandikwa  "Tafuta chochote hapa...." juu ya kurasa hii na endapo hujapata katika kiboksi hiko basi wasiliana na wafamasia wa ULY CLINIC maelezo zaidi kuhusu dawa.

​

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri na tiba kwa kubofya linki ya 'Mawasiliano yetu' au 'Pata tiba' chini ya tovuti hii

bottom of page