top of page

Dawa

ULY CLINIC inakutahadharisha kuwa matumizi ya dawa pasipo ushauri wa daktari yanaweza kuleta madhara makubwa mwilini mwako.

 

Siku zote wasiliana na daktari wako kwa elimu na ushauri wa dawa gani na namna ya kutumia dawa inayoendana na hali yako halisi kama mbadala ya kujichukulia hatua mwenyewe.

​

Bonyeza 'Soma zaidi ' kwenye dawa unayohitaji kuanza kusoma kuhusu dawa hiyo..

Vildaglipitin

Vildaglipitin

Ni dawa ya inayotumika katika tiba ya ugonjwa wa kisukari aina ya pili, ipo kwenye kundi la dawa linaloitwa dipeptidyl peptidase-4 (DPP-4).

Dawa Buformin

Dawa Buformin

Ni dawa ya kumeza inayotumika katika matibabu ya ugonjwa wa kisukari, dawa hii ipo kwenye kundi la dawa linaloitwa Biguanide.

Dawa Amlodipine

Dawa Amlodipine

Ni aina ya dawa iliyo kwenye kundi la dawa za kushusha shinikizo la juu la damu linaloitwa kalisimau chaneli bloka, hutumika katika matibabu ya shinikizo la juu la damu(haipatensheni) na anjaina.

Tolazamide

Tolazamide

Tolazamide ni dawa inayotumika katika matibabu ya kisukari na ipo kwenye kundi la kizazi cha kwanza cha dawa za sulfonylurea.

Dawa Metformin

Dawa Metformin

Ni dawa ya kundi la biguanidi inayotumika hasa kudhibiti kisukari cha aina ya pili kwa kusaidia kupunguza kiwango cha sukari kwenye damu, huku ikitumiwa kwa kufuata dozi na maelekezo ya mtoa huduma za afya.
Kwa kuwa matumizi yake yanaweza kuhitaji kuzingatia hali ya figo, dawa nyingine anazotumia mgonjwa na hali yake ya kiafya, ni muhimu kuitumia kwa usahihi na kutofautisha madhara ya kawaida na dalili zinazohitaji matibabu ya haraka.

Hujapata dawa unayotafuta?

 

Endapo hujapata dawa unayotafuta andika katika kiboksi kilichoandikwa  "Tafuta chochote hapa...." juu ya kurasa hii na endapo hujapata katika kiboksi hiko basi wasiliana na wafamasia wa ULY CLINIC maelezo zaidi kuhusu dawa.

​

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri na tiba kwa kubofya linki ya 'Mawasiliano yetu' au 'Pata tiba' chini ya tovuti hii

bottom of page