top of page

Mwandishi:

Mhariri:

Dkt. Sospeter M, MD

Dkt. Charles W, MD

9 Juni 2020 09:38:10

Vihatarishi vya kupata kisukari

Vihatarishi vya kupata kisukari

Vihatarishi vya kupata ugonjwa wa kisukari vinajumuisha,uzito, maeneo mafuta yalipohifadhiwa mwilini, kutofanya kazi za kushughulisha mwili, historia kwenye familia,historia ya kisukari cha ujauzito, sindromu ya polisistik ovarian. Maelezo kwa undani yanapatikana hapa chini


Uzito

Kuwa na uzito mkubwa kunakuweka hatarini kupata kisukari aina ya 2, jinsi unavyokuwa na mafuta mengi mwilini upinzani katika ufanyaji kazi wa homoni ya insulini huongezeka. Ingawa haina maaana unatakiwa uwe na uzito mkubwa ili upate kisukari ila hata mtu mwembamba anaweza kupata kisukari hiki aina ya 2.


Maeneo ya kuhifadhi mafuta

Kama mwili wako umehifadhi mafuta sehemu za kuta za tumbo (mwonekano wa kuwa na kitambi) huwa ni kihatarishi cha kupata kisukari zaidi ya mtu mwenye mafuta haya sehemu nyinginezo kama mapaja na nyonga.



Kutofanya kazi

Kutofanya kazi za Kuushughulisha mwili ili utoe jasho kunaongeza hatari ya kupata kisukari aina ya 2, pia hata wale wanaofanya kazi za ofisini na wakirudi nyumbani hawafanyi mazoezi wanawekwa kwenye kundi hili la kutofanyakazi. Kufanya kazi au mazoezi kunasaidia chembe hai za misuli ya mwili kuongeza utumiaji wa sukari(glukosi) na homini ya insulin.


Historia ya ugonjwa wa kisukari aina ya 2 kwenye familia

Kama mzazi au watoto wana kisukari aina hii ya 2 basi unakihatarishi cha kupata kisukari katika maisha yako pia.


Utaifa

Asili ya mtu. Watu weusi-wa Afrika, wa Hispania, wa Marekani, wa Hindi na wa Asia wapo hatarini zaidi kupata kisukari aina ya 2


Umri

Umri zaidi ya miaka 45 kisukari aina hii ya pili hutokea sana na hii ni kwa sababu labda watu katika umri huu hufanya mazoezi kidogo na pia wanapoteza misuli na kuongezeka uzito sana. Kisukari aina hii kinaongezeka sana kwa vijana wadogo(chini ya umri huu) pia katika karne hizi


Kisukari wakati wa ujauzito

Kama ulipata kisukari wakati wa ujauzito basi kisukari hicho huweza kuendelea kwa baadhi ya wanawake na endapo umejifungua mtoto zaidi ya kilo 4 basi pia inakuweka hatalini kupata kisukari aina ya 2


Ugonjwa wa Polycystic ovarian syndrome

Hutokea kwa wanawake , ugonjwa huu husababisha dalili nyingi kama vile kuwa na vipindi vya hedhi katikati ya mzunguko wa hedhi, kuwa na nywele nyingi kama mwanaume(ndevu n.k) na uzito kupita kiasi huongeza hatari ya kupata kisukari aina hii ya 2.

Imeboreshwa

11 Desemba 2021 14:20:36

Uly clinic inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote dhidi ya afya yako.

Wasiliana na daktari wa ULY clinic kwa kubonyeza 'Pata Tiba' au kwa kupiga namba za simu chini ya tovuti hii.

Rejea za mada hii;

  1. Tessier D, Meneilly GS. Diabetes management in the elderly. In: Gerstein HC, ed. Evidence-based diabetes care. Hamilton: BC Decker Inc., 2001, pg. 370–9.

  2. Lipska KJ, De Rekeneire N, Van Ness PH, et al. Identifying dysglycemic states in older adults: Implications of the emerging use of hemoglobin A1c. J Clin Endocrinol Metab 2010;95:5289–95.

  3. Crandall J, Schade D, Ma Y, et al. The influence of age on the effects of lifestyle modification and metformin in prevention of diabetes. J Gerontol A Biol Sci Med Sci 2006;61:1075–81.

  4. Chiasson JL, Josse RG, Gomis R, et al. Acarbose for prevention of type 2 diabetes mellitus: The STOP-NIDDM randomised trial. Lancet 2002;359:2072–7.

  5. DREAM (Diabetes REduction Assessment with ramipril and rosiglitazone Medication) Trial Investigators, Gerstein HC, Yusuf S, et al. Effect of rosiglitazone on the frequency of diabetes in patients with impaired glucose tolerance or impaired fasting glucose: A randomised controlled trial. Lancet 2006;368:1096– 105.

  6. Inzucchi SE, Viscoli CM, Young LH, et al. Pioglitazone prevents diabetes in patients with insulin resistance and cerebrovascular disease. Diabetes Care 2016;39:1684–92.

  7. Kronsbein P, Jorgens V, Muhlhauser I, et al. Evaluation of a structured treatment and teaching programme on non-insulin-dependent diabetes. Lancet 1988;2:1407–11.

  8. Wilson W, Pratt C. The impact of diabetes education and peer support upon weight and glycemic control of elderly persons with NonInsulin Dependent Diabetes Mellitus (NIDDM). Am J Public Health 1987;77:634–5.

  9. Braun AK, Kubiak T, Kuntsche J, et al. SGS: A structured treatment and teaching programme for older patients with diabetes mellitus–a prospective randomised controlled multi-centre trial. Age Ageing 2009;38:390–6.

  10.  Fagan PJ, Schuster AB, Boyd C, et al. Chronic care improvement in primary care: Evaluation of an integrated pay-for-performance and practice-based care coordination program among elderly patients with diabetes. Health Serv Res 2010;45:1763–82.

  11. McGovern MP, Williams DJ, Hannaford PC, et al. Introduction of a new incentive and target-based contract for family physicians in the UK: Good for older patients with diabetes but less good for women? Diabet Med 2008;25:1083–9.

  12. Maar MA, Manitowabi D, Gzik D, et al. Serious complications for patients, care providers and policy makers: Tackling the structural violence of First Nations people living with diabetes in Canada. Int Indigenous Policy J 2011;21:http://ir.lib.uwo.ca/iipj/vol2/iss1/6. Article 6.Imechukuliwa 05.06.2020

  13.  Jacklin KM, Henderson RI, Green ME, et al. Health care experiences of Indigenous people living with type 2 diabetes in Canada. CMAJ 2017;189:E106– 12.

  14. Chandler MJ, Lalonde C. Cultural continuity as a protective factor against suicide in First Nations Youth. Horizons 2008;10:68–72.

  15. Oster RT, Grier A, Lightning R, Mayan MJ, Toth EL. Cultural continuity, traditional Indigenous language, and diabetes in Alberta First Nations: A mixed methods study. Int J Equity Health 2014;13:92. doi:10.1186/s12939-014- 0092-4.

  16. Truth and Reconciliation Commission of Canada. Truth and reconcilliation commission of Canada: calls to action. Winnipeg, MB: Truth and Reconciliation Commission of Canada 2012. 2015. http://www.trc.ca/websites/ trcinstitution/File/2015/Findings/Calls_to_Action_English2.pdf.Imechukuliwa 05.06.2020

  17.  Yu CH, Zinman B. Type 2 diabetes and impaired glucose tolerance in aboriginal populations: A global perspective. Diabetes Res Clin Pract 2007;78:159– 70.

  18. Gracey M, King M. Indigenous health part 1: Determinants and disease patterns. Lancet 2009;374:65–75.

  19. Chronic Disease Surveillance and Monitoring Division, Centre for Chronic Disease Prevention and Control. Diabetes in Canada: Facts and figures from a public health perspective. Ottawa, ON: Public Health Agency of Canada, 2011 http://www.phac-aspc.gc.ca/cd-mc/publications/diabetes-diabete/facts -figures-faits-chiffres-2011/index-eng.php. Imechukuliwa 05.06.2020

  20. Turin TC, Saad N, Jun M, et al. Lifetime risk of diabetes among first nations and non-first nations people. CMAJ 2016;188:1147–53.

  21. Singer J, Putulik Kidlapik C, Martin B, et al. Food consumption, obesity and abnormal glycaemic control in a Canadian Inuit community. Clin Obes 2014;4:316– 23.

bottom of page