Imeandikwa na daktari wa ULY CLINIC
​
Kubanduka kwa ngozi ya kiganja cha mkono
​
Kubanduka kwa ngozi ya kiganja cha mkono kitabibu ikifahamika kwa jina la Keratolisis eksifoliativa au jina jingine la lamela dishaidrosis ni udhaifu wa ngozi ya kiganja cha mkono inayopelekea ngozi kubanduka. Tatizo hili hujirudia mara kadhaa na huweza kuathiri vidole vya mkono, kanyagio na huamswha sana kwa watu wengi kwenye majira ya kiangazi au hali ya hewa ya ujoto.
​
Tatizo la keratolisis eksifolietiva huchanjanywa maranyingi na ugonjwa wa dermataitis ya kiganja cha mikono/kanyagio (pumu ya ngozi), kwa kawaida demataitisi huwa inasababisha ngozi kuwa kavu/kukauka
Ni nani anayepata tatizo hili?
Hutokea kwa vijana wadogo wenye nguvu na wakati mwingine hutembea kwenye familia fulani
Nini husababisha tatizo la keratolisis eksfoliativa?
​
Kisababishi cha keratolisis eksfolietiva huwa hakifahamiki, endapo magamba yakitolewa kwenye kiganja cha mkono na kutazamwa kwa hadubini, seli za ngozi huonyesha kuvunjwa kwa ukuta wa nje ya ngozi ujulikanao kama stratamu corneum kwa sababu inayohisiwa kuwa seli za ukuta huu kutengana kabla ya wakati wake kufika. Tatizo hili bado halifahamiki endapo linahusiana na madhaifu ya vinasaba au la.
Dalili
​
Dalili zake huonekana pale ngozi inapochokozwa na sabuni, maji, dawa na vimiminika vya kusafishia vifaa mbalimbali na huweza kuambatana na tatizo la kutokwa na jasho.
Waathirika wa tatizo hili mara chache sana hutafuta msaada wa kitabibu. Dalili huwa pamoja na;
​
-
Kutokea kwa lengelenge lenye hewa kwa ndani kwenye viganja au vidole vya mikono
-
Kutokuwa na miwasho kabisa na kwa nadra kupata miwasho kiasi
-
Kujirudia kwa tatizo kila baada ya wiki chache kupita
​
Vipimo
​
Namna ya tatizo linavyotambuliwa
​
Tatizo la Keratolisis Eksifoliativa hutambulika kwa kuchunguzwa tu kwa macho na mara nyingi huwa hakuna haja ya kufanya vipimo.
Hata hivyo vipimo vifuatavyo vinaweza fanyika ili kumsaidia daktari kufahamu zaidi kuhusu tatizo lako na kutofautisha na matatizo mengine yanayofanana sana na hili;
​
-
Kipimo cha Biopsy kutoka kwenye ngozi inayobanduka
-
Kipimo cha kupima fangasi kutoka kwenye magamba ya ngozi
-
Kipimo cha pachi kufahamu kuhusu aleji mbalimbali kwenye ngozi
​
Magonjwa mengine yanayofanana na tatizo hili ni yapi?
​
Magonjwa haya yaliyoorodheshwa yanaweza kusababisha pia ngozi kubanduka, daktari atayatofautisha kwa kukuuliza maswali mbalimbali pamoja na vipimo kabla ya kuanza matibabu. (Bonyeza kusoma zaidi kuhusu ugonjwa unaofanana kwa kubonyeza maneno yaliyopigiwa mstari)
​
-
Demataitizi ya ngozi ikiwa pamoja na kontakti demataitis
-
Pompoliksi- huwa na dalili ya mwasho na malengelenge ya maji
-
Soriasisi ya Viganja vya mikono na miguu- huacha makovu makovu kwenye ngozi
-
Tinea manuum- Kipimo cha culture huwa chanya kwa fangasi
-
Keratodema ya viganja vya mikono/miguu
-
Epidemilosis bulosa simpleksi- hutokea na kuleta malengemakubwa yenye maji
Matibabu ya keratolisis Eksifolietiva
Vitu vifuatavyo vinaweza kusaidia endapo tatizo hili limetokea;
​
-
Kujikinga na visababishi/viamsha tatizo kama vilivyotajwa hapo juu kwa kuvaa glavu au vitu vingine vya kukinga kugusana na kemikali hizo kwenye mikono yako
-
Kutumia mafuta ya krimu yenye yurea, laktiki asidi au silicone kupaka kwenye ngozi
-
Matumizi ya Acitretin
-
Matibabu ya mionzi na dawa za kemotherapi
​
Kumbuka matibabu ya kutumia dawa jamii ya corticosteroidi na dawa za fangasi huwa hayasaidii wagonjwa wenye tatizo hili.
Mambo ya kufahamu
​
Wakati mwingine matibabu yanaweza kukusaidia au yasikusaidie kabisa, hata hivyo tatizo hili huwa haliambatani na ugonjwa wowote ndani ya mwili au kusababisha matatizo mengine ndani ya mwili isipokuwa hali ya kujihisi sio wa kawaida hivyo kukuathiri kisaikolojia
ULY CLINIC inakushauri siku zote ufuate ushauri wa daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kaifya
Soma zaidi kuhusu magonjwa mengine ya ngozi kwa kubonyeza hapa
Bonyeza hapa kusoma kuhusu kubanduka ngozi kwa ujumla
​
Bonyeza hapa kurudi kwenye magonjwa mengine ya ngozi
​
Imeboreshwa mara ya mwisho, 1.11.2020
Rejea za mada hii;
​
-
Dermnets NZ. Keratolysis exfoliativa. https://dermnetnz.org/topics/keratolysis-exfoliativa/. Imechukuliwa 25.10.2020
-
Keratolysis Exfoliativa mayoclinic. https://cleanexperts.com.au/docs/616fa2-keratolysis-exfoliativa-mayo-clinic.Imechukuliwa25.10.2020
-
Dermatology advisor. Keratolysis exfoliativa. https://www.dermatologyadvisor.com/home/decision-support-in-medicine/dermatology/keratolysis-exfoliativa-lamellar-dyshidrosis-recurrent-focal-palmar-peeling-recurrent-palmar-peeling/Imechukuliwa 25.10.2020