Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
27 Oktoba 2020 07:14:29
Dawa ya Tigecycline
Tigecycline ni aina ya dawa mojawapo ya antibayotiki jamii ya tetracycline ambayo hutumika kupambana na Maambukizi mbalimbali kwenye mwili.Dawa hii huwa maarufu kwa jina la Tygacil
Mfumo wa dawa
Hupatikana katika mfumo wa;
Unga ambao hutumika kwa ajili ya sindano wenye uzito wa Milligramu 50 kwa chupa
Namna dawa inavyofanya kazi
Dawa jamii ya Tigecycline ikiwa pamoja na tetracycline hufanya kazi Ifuatayo kupambana na bakteria
Dawa hii hufanya kazi kwa kuzuia ukuaji wa bakteria kwa kuzuia utengenezaji wa protini kwenye bakteria
Dawa zilizo kundi moja na dawa hii
Dawa zingine zilizo kwenye kundi moja (Doxycline) na dawa hii ni;
Choltetracycline
Oxytetracycline
Tetracycline
Minocycline
Demecycline
Methacyxline
Rolitetracyxline
Kazi ya dawa
Hutumika kwenye matibabu ya magonjwa sugu ya ngozi
Hutumika kwenye matibabu ya Maambukizi ndani ya tumbo
Utofauti wa pekee wa dawa hii na dawa zingine kwenye kundi moja
Utofauti wa pekee wa dawa hii na dawa zingine za kwenye kundi hili la (Tetracycline)
Dawa hii nusu ya maisha ya dawa hii ni masaa27 tangu itumike mwilini
Dawa hii hutolewa kwa njia ya kinyesi zaidi ukilinganisha na mkojo
Dawa zisizopaswa kutumika na dawa hii
Dawa hii haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo;
Acitretin
Flibanserin
Lomitapide
Tretinoin
flibanserin
lomitapide
tretinoin
Aluminum hydroxide
Aminolevulinic acid
Amoxicillin
Ampicillin
Apalutamide
Atracurium
Avapritinib
Axitinib
Bismuth subsalicylate
Bosutinib
Calcium acetate
Calcium carbonate
Calcium chloride
Calcium citrate
Calcium gluconate
Carbonyl iron
Cisatracurium
Cobimetinib
Dicloxacillin
Eliglustat
Wagonjwa wasiopaswa kutumia dawa hii
Dawa hii haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao
Wagonjwa wenye aleji na dawa hii au jamii ya dawa za tetracycline
Wagonjwa wa ini
Na mama mjamzito kwenye miezi 6 ya mwishoni
Tahadhari ya dawa hii
Dozi yake inapaswa kupunguzwa kwa mgonjwa mwenye shida ya figo
Huweza kuharibu rangi ya meno kwa mtoto kuanzia kwenye miezi 6 ya mwisho ya mimba hadi miaka 8
Matumizi kwa mama mjamzito na anayenyonyesha
Kwa mama mjamzito na anayenyonyesha
Dawa hii ipo kwenye kundi D la usalama kwa mama mjamzito
Dawa hii inaweza kutumika kwenye miezi mitatu ya kwanza ya ujauzito na baada ya hapohairuhusiwi kutumika
Inaweza kutumika kwa mama anayenyonyesha sababu hakuna madhara yeyote yaliyoripotiwa
Maudhi ya dawa hii
Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hii ni;
Kizunguzungu
Kichefuchefu
Kutapika
Homa
Kichwa Kuuma
Je endapo utasahau dozi yako ufanyaje?
Endapo ukisahau kutumia dozi yako tumia mara pale utakapokumbuka na endapo muda wa dozi nyingine umekaribia acha dozi uliyoisahau na endelea na dozi yako kama ulivyopangiwa na daktari wako
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023 16:54:56
Rejea za mada hii:-