top of page

Dawa

ULY CLINIC inakutahadharisha kuwa matumizi ya dawa pasipo ushauri wa daktari yanaweza kuleta madhara makubwa mwilini mwako.

 

Siku zote wasiliana na daktari wako kwa elimu na ushauri wa dawa gani na namna ya kutumia dawa inayoendana na hali yako halisi kama mbadala ya kujichukulia hatua mwenyewe.

​

Bonyeza 'Soma zaidi ' kwenye dawa unayohitaji kuanza kusoma kuhusu dawa hiyo..

Dawa Aminophylline

Dawa Aminophylline

Aminophylline ni bronchodilator inayotumika kudhibiti pumu ya kifua na ugonjwa sugu wa kuziba kwa njia za hewa (COPD) kwa kupanua njia za hewa, lakini inaweza kusababisha mapigo ya moyo kwenda haraka, arithimia, na kizunguzungu. Dozi lazima ichaguliwe na daktari, ikizingatia umri, uzito na hali ya afya ya mgonjwa.

Dawa Promethazine

Dawa Promethazine

Promethazine ni antihistamine na antitussive inayotumika kupunguza allergy, kichefuchefu, na kikohozi kikavu, lakini inaweza kusababisha usingizi mkali na madhara makubwa kwa watoto, wajawazito, na wanaonyonyesha. Inapaswa kutumika tu chini ya uangalizi wa daktari na kwa dozi sahihi.

Dawa Codeine

Dawa Codeine

Codeine ni dawa ya opioid inayotumika kutuliza maumivu ya wastani na kikohozi kikavu lakini ina hatari ya utegemezi na maudhi makubwa. Inapaswa kutumiwa kwa uangalizi wa daktari, hasa kwa wajawazito, wanaonyonyesha na watoto.

Dawa Diclofenac

Dawa Diclofenac

Ni dawa ya maumivu na uvimbe kundi la NSAID inayotumika kutibu maumivu ya wastani hadi makali kama ya viungo, hedhi na baridi yabisi. Hutumika kwa uangalifu mkubwa hasa kwa wajawazito (hairuhusiwi kuanzia wiki ya 30), wagonjwa wa moyo, tumbo na figo kwa sababu ya hatari ya madhara makubwa.

Dawa Ketoprofen

Dawa Ketoprofen

Ketoprofen ni dawa ya kundi la NSAIDs inayotumika kupunguza maumivu, uvimbe na homa kwa magonjwa kama maumivu ya misuli, viungo na hedhi. Haitibu chanzo cha ugonjwa, hivyo inapaswa kutumiwa kwa uangalizi wa mtaalamu ili kuepuka madhara hasa ya tumbo, figo na moyo.

Hujapata dawa unayotafuta?

 

Endapo hujapata dawa unayotafuta andika katika kiboksi kilichoandikwa  "Tafuta chochote hapa...." juu ya kurasa hii na endapo hujapata katika kiboksi hiko basi wasiliana na wafamasia wa ULY CLINIC maelezo zaidi kuhusu dawa.

​

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri na tiba kwa kubofya linki ya 'Mawasiliano yetu' au 'Pata tiba' chini ya tovuti hii

bottom of page