Imeandikwa na famasia wa ULY-Clinic
Dawa ya Diclofenac
Ni dawa ya kutibu maumivu jamii ya NSAID’s, hupatikana kwa mfumo wa
-
Kidonge kilichoungwa na madini ya Potasiamu. Kidonge kinaweza kuwa na chenye miligramu 50, 25, 75, 100
-
Tembe za miligramu 18, 25 na 35
-
Unga , miligramu 37.5 kwa kila mililita moja ya maji
-
Jeli au krimu ya kupaka
Rangi ya kidonge
Kidonge cha diclofenac(diklofenaki) kinaweza kuwa cha rangi aina tofauti kama brauni, nyeupe, njano, pinki n.k
Majina mengine ya dawa hii
Cataflam, Voltaren-XR, Dyloject, Cambia, Zipsor, Zorvolex, Diclopa, Declofenac
Matumizi
-
Kutibu athraitis ya ryumatoid (baridi yabisi)
-
Osteoathraitiz
-
Spondilaitiz ya ankailozing
-
Maumivu ya kiasi hadi wastani
Maudhi ya dawa hii
-
Kuvimba kwa tumbo na kujamba
-
Maumivu ya tumbo na Maumivu ya kukata kwa tumbo
-
Haja ngumu
-
Kuharisha
-
Kuvimba
-
Vidonda vya tumbo na kutokwa damu tumboni
-
Upele
-
Masikio kupiga kelele(tinitas)
-
Hepataitis ya ghafla
-
Agranulosaitosis
-
Anemia ya aplastiki
-
Hepataitis isiyo na dalili
-
Kupanda kwa kiwango cha BUN zaidiya 40 kwa kila desilita moja
-
Kolestaisi
-
Hepatitis sugu
-
Kupungua kwa hemoglobin
-
Hepataitis ya kuua ya fulminat
-
Anemia ya hemolitiki
-
Nekrosis ya hepatoselula
-
Manjano
-
Liukopeni
-
Sumu kwa figo
-
Kupandisha kiwango cha creatinine Zaidi ya miligramu 2 kwa kila desilita moja (2mg/dL)
-
Thrombosaitopenia
Tahadhari
Kwenye mfumo wa moyo
-
Dawa jamii ya NSAID’s huweza kuongeza hali ya magonjwa hatari ya moyo na matukio ya thrombotiki, infakisheni ya mayokadia, kiharusi, haya yote huweza kuua mtu.
-
Hatari huongezeka zaidi kulingana na muda wa matumizi
-
Wagonjwa walio na ugonjwa wa moyo au wenye kihatarishi cha ugonjwa wa moyo wapo hatarini zaidi
-
NSAID’s haziruhusiwi kutumika wakati wa upasuaji wa mishipa ya damu ya koronari(CABG)
Kwenye mfumo wa chakula
-
Dawa jamii ya NSAID’s huweza kuongeza hatari ya kutokwa damu tumboni, vidonda vya tumbo na kutoboa utumbo na tumbo ambapo mtu huweza kupoteza Maisha.
-
Madhara kwenye mfumo huu huweza kutokea ghafla bila ishara
-
Wazee wapo hatarini kupata madhara mabaya kwenye mfumo huu wa chakula.
Katazo
Marufuku: kutumika kwa watu weye mzio na dawa hii, wenye historia ya kupata madhara ya aspirini, kutibu wagonjwa waliofanyiwa au wanaotaka kufanyiwa upasuaji wa mishipa ya damu ya moyo ya koronari na wale wanaotokwa damu kwenye mfumo wa chakula.
Kwa wagonjwa walioferi figo kwa wastani au kabisa kipindi cha upasuaji, au wagonjwa wenye hatari ya kuishiwa damu.
Watu wenye historia ya mzio na protini ya bovin
Angalizo
Tumia dawa hii kwa umakini kwa wagonjwa hawa
-
Wenye bronkospazimu
-
Magonjwa ya moyo
-
Pofria ya hepatiki
-
Kuvuta sigara
-
Lupasi ya erizimatazi kwenye mfumo wa mwili
-
Thrombosaitoopenia
-
Kuferi kwa urojo wa mifupa
-
Agranulosaitosis
-
Anemia ya Aplastiki
-
Moyo ulioferi- NSAID’s huweza kusabaisha moyo kuferi kwa kutunza maji na chumvu na mwili kushindwa kuitikia dhidi ya dawa za kuchuja maji.
Matumizi ya diclofenac wakati wa Ujauzito na kunyonyesha
Matumizi ya dawa jamii ya NSAID’swakati wa ujauzito huweza kusababisha kufunga kwa arteriosus ya daktasi kabla ya wakati. Dawa hii inatakiwa kuacha kutumia endapo mimba ina wiki 30 na kuendelea.
Ugumba
Kutokana na ufanyajikazi wake, matumizi ya dawa za NSAID’s zinazofanya kazi na njia ya prostaglandins huweza kuchelewesha kutolewa kwa yai kwenye ovari, hii husababisha ugumba wa muda kwa wanawake. Tafiti kwa Wanyama na binadamu zimeonyesha pia kuchelewa kwa kutolewa kwa mayai kwa kutoka kwenye ovari. Hivyo kwa wanawake ambayo wanafanyiwa vipimo vya ugumba au kutaka Watoto wanaweza kufikiriwa kuacha tumia dawa hii kipindi hiki.
Matumizi ya Diclofenac wakati wa kunyonyesha
Tafiti zinaonekana kuwa kiwango kidogo cha diclofenac hupita na kuingia kwenye maziwa ya mama, lakini hakuna tafiti zinazoonyesha madhara kwa mtoto kutokana na kunyonya maziwa ya mama au madhara dhidi ya uzalishaji wa maziwa. Unapotoa dawah ii hakikisha kuwa faida ni kubwa kuliko madhara yanayoweza kujitokeza kwa mama au mtoto.
Endapo umesahau kunywa dozi
Kama umesahau kunywa dozi yako, unaweza kunywa mara tu unapokumbuka, isipokuwa endapo muda wa dozi ingine umeshafika unatakiwa kuruka hiyo dozi uliyosahau na kuendelea na dozi yako kama muda uliopangiwa.
ULY CLINIC inakukumbusha uwasiliane na daktari wako kabla ya kutumia dawa yoyote ile
Imeboreshwa 3.12.2020