Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
ULY CLINIC
31 Oktoba 2026, 15:23:37

Tofauti ya Vipele vya magonjwa hatari na vipele vya kawaida
Jibu kwa ufupi
Jibu kwa ufupi: Fanya kipimo cha glasi – vipele visivyofifia ukibonyeza glasi pamoja na homa ni dharura. Mgonjwa mwenye vipele na kuonekana mgonjwa sana – hospitali mara moja. Soma Vipele mwilini.
Maelezo
Vipele vya kawaida
Mgonjwa anaonekana mzima; homa kidogo au hakuna.
Vipele hufifia ukibonyeza.
Joto, mzio, wadudu, virusi vya kawaida, ukurutu – soma Upele mwilini.
Vipele vya hatari
Madoa yasiyofifia + homa – homa ya uti wa mgongo, sepsis; soma Homa ya uti wa mgongo.
Surua – homa, kikohozi, mafua, macho mekundu, vipele kuanzia usoni; soma Surua.
Mpox – malengelenge/usaha, mitoki kuvimba, homa; soma Mpox.
Dengue – homa kali, maumivu ya mifupa, madoa ya damu; soma Homa ya dengue.
SJS/TEN – malengelenge, ngozi kubanduka, vidonda mdomoni na machoni baada ya dawa mpya.
Mzio mkali – vipele + uvimbe wa uso/koo, kupumua kwa shida; soma Mzio mkali.
Kipimo cha glasi
Bonyeza glasi safi juu ya vipele.
Vikifichika (kufifia) – mara nyingi si vya hatari.
Visipofifia – dharura, hasa kukiwa na homa.
Nini cha kufanya
Andika dawa mpya ulizoanza.
Mtenge mgonjwa wa surua au mpox na wengine hadi uchunguzi.
Chanjo – surua-rubella kwa watoto.
Dalili za hatari
Hospitali MARA MOJA ukiona:
Vipele visivyofifia + homa.
Malengelenge, ngozi kubanduka, vidonda mdomoni/machoni.
Uvimbe wa uso au koo, kupumua kwa shida.
Mtoto mwenye vipele, homa na kulegea.
Lini umwone daktari
Vipele zaidi ya wiki 1.
Vipele vyenye usaha au vinavyoenea.
Vipele pamoja na homa ya siku kadhaa.
Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
1. Nitajuaje vipele ni hatari?
Visivyofifia kwa glasi, homa kali, malengelenge mengi au uvimbe wa uso.
2. Kipimo cha glasi kinafanyikaje?
Bonyeza glasi juu ya vipele; visivyofifia ni hatari.
3. Vipele vya surua vikoje?
Huanza usoni baada ya homa, kikohozi na macho mekundu.
4. Mpox ina vipele vya aina gani?
Malengelenge yanayogeuka usaha, pamoja na mitoki kuvimba.
5. Vipele baada ya dawa mpya?
Mwambie mtoa huduma mara moja.
6. Vipele vingi vya watoto ni hatari?
Vingi si hatari; angalia dalili za hatari.
Imeandikwa:
2 Aprili 2026, 17:07:17
ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.
Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.
Rejea za mada hii:
National Institute for Health and Care Excellence. Meningitis (bacterial) and meningococcal disease: recognition, diagnosis and management (NG240). London: NICE; 2024.
World Health Organization. Mpox – fact sheet. Geneva: WHO; 2024.
Ministry of Health, United Republic of Tanzania. Standard Treatment Guidelines and National Essential Medicines List (STG/NEMLIT), 7th edition. Dodoma: Ministry of Health; 2026.

