Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
ULY CLINIC
31 Oktoba 2026, 15:23:37

Fluconazole na magonjwa ya zinaa
Jibu kwa ufupi
Swali la mteja: "Habari daktari, naomba kujua kama fluconazole inaweza kutibu magonjwa ya zinaa?"
Jibu kwa ufupi: Hapana. Fluconazole hutibu fangasi ukeni, uumeni, kwenye korodani na mdomoni. Magonjwa ya zinaa yanahitaji dawa nyingine kulingana na chanzo. Soma Fluconazole katika tiba.
Maelezo
Fluconazole hutibu
Fangasi ukeni – muwasho, uchafu mweupe kama maziwa mgando, maumivu wakati wa tendo.
Fangasi uumeni na kwenye korodani.
Fangasi mdomoni na kooni.
Magonjwa ya zinaa ambayo fluconazole haitibu
Kaswende – bakteria; sindano.
Trikomona – vimelea; dawa ya aina ya metronidazole.
Malengelenge – virusi; dawa za kupunguza virusi.
HPV na VVU – virusi; huduma maalumu.
Kutofautisha kwa dalili (si kwa uhakika)
Uchafu mweupe mzito kama maziwa mgando, muwasho, bila harufu – mara nyingi fangasi.
Uchafu wa njano au kijani, wenye povu au harufu – trikomona au bakteria.
Usaha uumeni, kuungua ukikojoa – kisonono au klamidia.
Vidonda sehemu za siri – kaswende au malengelenge.
Nini cha kufanya
Pima kituo cha afya kabla ya kununua dawa – soma Uke kutoa usaha.
Mwenzi atibiwe pia kama ni ugonjwa wa zinaa.
Epuka ngono hadi wote mmalize dawa.
Pima VVU na kaswende ukiwa na ugonjwa wowote wa zinaa.
Tumia kondomu.
Dalili za hatari
Nenda kituo cha afya mara moja ukiwa na:
Maumivu ya tumbo la chini na homa.
Korodani kuvimba na kuuma.
Vidonda sehemu za siri.
Lini umwone daktari
Dalili hazipungui baada ya fluconazole.
Fangasi hujirudia mara 4 au zaidi kwa mwaka.
Mwenzi wako amegundulika na ugonjwa wa zinaa.
Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
1. Fluconazole inatibu kisonono?
Hapana. Kisonono kinahitaji antibiotiki maalumu.
2. Nina uchafu ukeni, nimeze fluconazole?
Pima kwanza – uchafu unaweza kuwa wa bakteria au trikomona.
3. Fangasi ukeni ni ugonjwa wa zinaa?
Kwa kawaida hapana, ingawa mara chache huenezwa kwa ngono.
4. Mwanaume anaweza kupata fangasi kutoka kwa mpenzi?
Ndiyo, mara chache – huwasha na kuwa na wekundu kwenye kichwa cha uume.
5. Fluconazole na metronidazole zinatofautiana?
Ndiyo – fluconazole ni ya fangasi; metronidazole ni ya trikomona na baadhi ya bakteria.
Imeandikwa:
2 Aprili 2026, 19:07:21
ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.
Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.
Rejea za mada hii:
Ministry of Health, United Republic of Tanzania. Standard Treatment Guidelines and National Essential Medicines List (STG/NEMLIT), 7th edition. Dodoma: Ministry of Health; 2026.
Workowski KA, et al. Sexually Transmitted Infections Treatment Guidelines, 2021. MMWR Recomm Rep. 2021;70(4):1–187.
Pappas PG, et al. Clinical practice guideline for the management of candidiasis: 2016 update by the IDSA. Clin Infect Dis. 2016;62(4):e1–50.

