top of page

Imeandikwa na daktari wa ULY CLINIC

​

Madhara ya kutumia dawa za kusimamisha uume pamoja na pombe

​

Dawa hizi zinafanya kazi kwa kushusha shinikizo la damu kwenye mapafu na kuongeza shinikizo la damu kwenye mishipa ya damu ya vein iliyo kwenye uume. Endapo dawa hizo zitatumika pamoja na pombe, shinikizo la damu linaweza kushuka chini mara dufu zaidi na hivyo mtu kupata madhara ya kizunguzungu kikali, kutokwa na jasho na maumivu ya kichwa. Mfano wa dawa ni Viagra(sildenafil), tadalafil, vardenafil.

​

Ushauri: Endapo unakunywa dawa zozote zile za dukani ni vema ukawasilaina na daktari wako, ili kuzuia madhara unayoweza kuyapata. Na pia ni vema ukaacha kutumia pombe wakati unatumia dawa mpaka umalize dozi nzima.

​

Imepitiwa 24.02.2020

​

Rejea

BNF 2018

bottom of page