top of page

Mwandishi: ULY CLINIC

​

Imeandikwa Juni, 2020

​

Madhara ya kutumia pombe na dawa za maumivu

​

Dawa za maumivu zipo kwenye makundi mbalimbali kulingana na jinsi zinavyofanya kazi. Dawa jamii ya NSAIDs  mfano Naproxen, Ibrupofen zikitumika pamoja na pombe huweza kuleta madhara ya kuvurugika kwa tumbo,  kuvia damu ndani ya tumbo na vidonda vya tumbo

​

Dawa jamii aina ya acetaminofeni ikijulikana kama paracetamol au panado endapo itatumika pamoja na pombe itashindwa kuchujwa kwenye ini kwa kuwa pombe hutawala ini kazi za ini. Hivyo dawa hii itakuwa nyingi kwenye damu na kusababisha ini kuharibika.

​

Dawa jamii ya opioid mfano codein na oxycodein ikitumika pamoja na pombe huleta maudhi makali kwenye mfumo wa upumuaji (kushusha mapigo ya upumuaji), usingizi mzito na mwisho ni kifo.

​

Imepitiwa 24.02.2023

​

Rejea

​

BNF  toleo la 2018

bottom of page