top of page

Mwandishi: ULY CLINIC

Mhariri: Dkt.Benjamin Lugonda, MD

​

Imeandikwa 06.04.2020

​

Dawa ambazo ni mwiko kunywa endapo umekunywa pombe

Watu wengi wamekuwa wanauliza maswali wataalamu wa afya, mimi pia nimeshakutana na swali hili mara nyingi,  wakati mimi mwenyewe nilijiuliza swali kuhusu dawa gani ambazo hazitakiwi kutumika pamoja na pombe?  na ili nipate kuwashauri wagonjwa wateja wangu na wasomaji vizuri nimeamua kuandaa makala hii ili kila atakayeuliza swali nimrejeshe kwenye mada hii.
 

Swali jingine

 

Ni kwa muda gani sipaswi kutumia pombe mara baada ya kunywa dawa?

 

Au ni muda gani unatakiwa kupita mara baada ya kunywa dawa ili ninywe pombe?

 

Mjadala huu umejibu maswali hayo vizuri;

​

Nianze na swali la ni dawa gani ambazo ni mwiko/ hazitakiwi kutumiwa endapo umekunywa pombe?

​

Jibu

Dawa zilizo kwenye makundi yaliyoorodheshwa chini hazitakiwi kutumika wakati umekunywa pombe au kwa mtu ambaye anatarajia kunywa pombe baadae baada ya kunywa dawa.

 

Dawa hizi hazitakiwi kutumika na pombe kwa sababu mtu anaweza kupata madhara au maudhi mbalimbali endapo atatumia dawa kwenye kipindi hiko. Bofya kusoma madhara katika kila kundi na mfano wa dawa.

​

​

Kwanini dawa nyingi hazitakiwi kutumiwa pamoja na pombe?

​

Zipo sababu mbalimbali zikiwa pamoja na;

​

  • Pombe huweza kudhoofisha uwezo wa dawa kufanya kazi yake ipasavyo

  • Pombe hufanya dawa iwe sumu mwilini

  • Pombe huongeza ukubwa wa maudhi ya dawa

  • Dawa ikichanganywa na pombe hutengeneza maudhi  mabaya Zaidi kuliko yale yanayofahamika kusababishwa  na dawa

 

Swali jingine

 

Ni muda gani natakiwa nisitumie pombe mara baada ya kunywa dawa?

 

Kujibu swali hili inahitaji kujibu swali la hapa chini

​

Ni kwa muda gani pombe inakaa kwenye damu?

​

Jibu

Kasi ya kusafisha pombe kwenye damu inayofanywa na Ini pamoja na figo inategemea jinsia ya mtu, uzito, umri, hali ya kiafya, kiwango cha shughuli za metaboliki, kiwango na aina ya pombe iliyotumiwa, dawa ulizotumia pamoja na pombe, na aina au kiasi cha chakula ulichotumia pamoja na pombe.

​

Kwa wastani inachukua saa moja(1) kwa mwili kuondoa uniti moja ya pombe kwenye damu

 

Uniti moja ya pombe hupatikana kwa kuzidisha  kiasi cha kilevi kwenye pombe mara ujazo wa pombe( kwa mililita) kisha gawanya kwa elfu moja(1000). Mfano bia ya kawaida ina asilimia 6%  ya kilevi na ujazo wake kwenye chupa ni mililita 300. Pombe hii itakuwa na uniti za kilevi ambazo ni 1.8 yaani  (6*300)/1000 

​

Hivyo mtu akinywa bia moja kama iliyotolewa mfano hapo juu itachukua takribani masaa mawili kuisha/kutolewa mwilini.

​

Mfano mwingine Mtu anayetumiwa wine ya dompo endapo atakunywa chumba nzima, yenye mililita 750 yenye kilevi asilimia18%,  uniti atakazokuwa ametumia ni (18*750)/1000 ambapo jibu litakuwa ni unit 13.5. Hivyo pombe itaisha kwenye damu baada ya masaa 13 hadi 14.

​

Mfano wa tatu, endapo mtu ametumia bia yenye mililita za ujazo wa 300 na kiwango cha pombe ni asilimia 6 na ametumia bia tatu. Uniti alizotumia itakuwa sawa na (6*300*3)/1000 ambapo jibu ni uniti 5.4 hivyo itachukua takribani masaa matano hadi sita kwa mwili kusafisha kiwango cha bia tatu katika damu.

​

Makala imejibu swali la muda gani  unatakiwa kupita kablla ya kunywa dawa endapo nimekunywa pombe.

​

Je ni muda gani unatakiwa kupita baada ya kunywa dawa ili unywe pombe?

​

Swali hili jibu lake ni rahisi, Muda unategemea  umri wa dawa kuishi kwenye damu. Hivyo ni lazima kujua urefu wa maisha ya dawa kwenye damu, yaani dawa inakaa muda gani kwenye damu kabla ya kuisha kabisa.

​

Kila dawa ina umri wake wa kuishi kwenye damu kabla ya kiwango kuwa kidogo au kuisha kabisa kwa kutolewa na figo kama mkojo au kuvunjwa na Ini. Unaweza kusoma umri wa dawa kuishi kwenye dawa husika

​

Inashauriwa usitumie pombe wakati wa kunywa dawa mpaka umalize dozi kwa usalama wako

 

Endapo unahitaji maelezo zaidi, wasiliana kwa namba za simu chini ya tovuti hii. Kabla ya kuwasiliana bofya namba hizo kupata maelezo ya namna ya kuwasiliana nasi

​

Pakua application ya ULY CLINIC kusoma makala zaidi na usisahau kutoa mrejesho wako.

​

Imeboreshwa: 12.06.2023

 

Rejea za mada hii;

 

  1. BNF toleo la 2018

  2. ULY CLINIC dawa mbalimbali na ombe

  3. National Institute on Alcohol Abuse and Alcoholism: "Harmful Interactions: Mixing Alcohol with Medicines."

  4. Substance Abuse and Mental Health Services Administration: "Alcohol, Medication, and Older Adults."

  5. CDC: "Alcohol Use."

  6. Harmful Interactions.Mixing Alcohol With Medicines. https://www.niaaa.nih.gov/publications/brochures-and-fact-sheets/harmful-interactions-mixing-alcohol-with-medicines. Imechukuliwa 06.04.2021

bottom of page