top of page

Dawa

ULY CLINIC inakutahadharisha kuwa matumizi ya dawa pasipo ushauri wa daktari yanaweza kuleta madhara makubwa mwilini mwako.

 

Siku zote wasiliana na daktari wako kwa elimu na ushauri wa dawa gani na namna ya kutumia dawa inayoendana na hali yako halisi kama mbadala ya kujichukulia hatua mwenyewe.

Bonyeza 'Soma zaidi ' kwenye dawa unayohitaji kuanza kusoma kuhusu dawa hiyo..

Dawa ya Terazosin

Dawa ya Terazosin

Terazosin ni dawa mojawapo ya kutibu shinikizo la juu la damu Iliyopo kwenye kundi la dawa linaloitwa Alpha Risepta Antagonisti. Dawa hii huwa maarufu kwa jina la Hytrin

Sodium Nitroprusside

Sodium Nitroprusside

Sodium Nitroprusside ni dawa Iliyopo kwenye kundi la dawa linaloitwa Vasodilator inayotumika kushusha shinikizo la juu la damu.

Mecamylamine

Mecamylamine

Mecamylamine ni dawa ya kutibu shinikizo la juu la damu. Dawa hii iliyo maarufu kwa jina la Inversine hupatikana kama kidonge cha miligramu 2.5 na inaweza kutumika pamoja au pasipo chakula mara mbili au tatu kwa siku kama utakavyoelekezwa na kushauriwa na Daktari.

Guanfacine

Guanfacine

Guanfacine ni dawa mojawapo ya kutibu shinikizo la juu la damu Iliyopo kwenye kundi la dawa linaloitwa Alpha 2 Adrenergic Agonisti. Dawa hii huwa maarufu kwa majina ya Intuniv na Tenex

Clonidine

Clonidine

Clonidine ni dawa mojawapo ya kutibu shinikizo la juu la damu Iliyopo kwenye kundi la dawa linaloitwa Alpha II Agonisti . Dawa hii huwa maarufu kwa majina ya Catapres na Catapres-TT

Aliskiren

Aliskiren

Aliskiren ni aina ya dawa mojawapo ya kutibu shinikizo la juu la damu Iliyopo kwenye kundi la dawa linaloitwa Renin inhibita. Dawa hii iliyo maarufu kwa jina la Tekturna huwa na rangi ya pinki au nyekundu isiyokolea hata hivyo mara nyingi hutegemea aina ya kiwanda kinachotengeneza dawa

Ethacrynic Acid

Ethacrynic Acid

Ni dawa mojawapo ya kutibu kuvimba kwa sehemu za mwili kama miguu. Dawa hii ipo kwenye kundi la dawa za Loop Diuretics nahuwa maarafu kwa jina la Edecrin

Indapamide

Indapamide

Ni dawa mojawapo ya kutibu shinikizo la juu la damu pamoja na kuondoa uvimbe unaotokana na kuvia kwa maji kwenye chemeb za mwili . Dawa hii ipo kwenye kundi la dawa za Thiazide Diuretics

Nebivolol

Nebivolol

Nebivolol ni dawa mojawapo ya kutibu shinikizo la juu la damu iliyoko katika kundi la dawa linaloitwa beta bloka. Dawa hii huwa maarufu pia kwa jina la Bystolic na hupatikana katika mfumo wa kidonge.

Ramipril

Ramipril

Ramipril ni dawa mojawapo ya kutibu shinikizo la juu la damu iliyo katika kundi la dawa linaloitwa angiotensini konventing enzaimu inhibita- ACEIs. Dawa hii huwa maarufu pia kwa jina la Altace.

Carteolol

Carteolol

Carteolol ni dawa mojawapo ya kutibu shinikizo la juu la damu iliyoko katika kundi la dawa linaloitwa beta bloka. Dawa hii huwa maarufu pia kwa jina la Ocupress.

Valsartan

Valsartan

Valsartan ni dawa mojawapo ya kutibu shinikizo la juu la damu iliyoko katika kundi la dawa linaloitwa angiotensini II risepta antagonist (ARBs). Dawa hii huwa maarufu pia kwa jina la Diovan au Prexxartan.

Hujapata dawa unayotafuta?

 

Endapo hujapata dawa unayotafuta andika katika kiboksi kilichoandikwa  "Tafuta chochote hapa...." juu ya kurasa hii na endapo hujapata katika kiboksi hiko basi wasiliana na wafamasia wa ULY CLINIC maelezo zaidi kuhusu dawa.

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri na tiba kwa kubofya linki ya 'Mawasiliano yetu' au 'Pata tiba' chini ya tovuti hii

bottom of page