top of page

Dawa

ULY CLINIC inakutahadharisha kuwa matumizi ya dawa pasipo ushauri wa daktari yanaweza kuleta madhara makubwa mwilini mwako.

 

Siku zote wasiliana na daktari wako kwa elimu na ushauri wa dawa gani na namna ya kutumia dawa inayoendana na hali yako halisi kama mbadala ya kujichukulia hatua mwenyewe.

Bonyeza 'Soma zaidi ' kwenye dawa unayohitaji kuanza kusoma kuhusu dawa hiyo..

Pindolol

Pindolol

Pindolol hutumika kwenye matibabu ya kushusha shinikizo la juu la damu, inaweza kutumika kama yenyewe au pamoja na dawa jamii ya thiazide diuretics.

Penbutolol

Penbutolol

Penbutolol ni dawa ya kutibu shinikizo la juu la damu iliyo kwenye kundi la beta bloka isiyo na mwingiliano kwenye mfumo wa ki autonomiki.

Propranolol

Propranolol

Propranolol ni dawa mojawapo ya kutibu shinikizo la juu la damu iliyo kwenye kundi la beta bloka.

Glyclopyramide

Glyclopyramide

Glycopyramide ni dawa inayotumika kuthibiti kupanda kwa kiwango cha sukari wkenye damu kwa wagonjwa wa kisukari aina ya Pili. Dawa hii ipo katika kundi la dawa linaloitwa sulfonylurea kizazi cha pili na huweza kusababisha mgonjwa akakojoa mara kwa mara.

Voglibose

Voglibose

Voglibose ni ni dawa inayotumika kushusha kiwango cha sukari kwenye damu na kuhakikisha kinabaki kwenye kiwango cha kawaida kwa wagonjwa wenye kisukari.

Metoprolol

Metoprolol

Metoprolol ni dawa inayotumika kutibu shinikizo la juu la damu, angina na kupunguza hatari ya kifo inayotokana na infaksheni ya mayokadia.

Miglitol

Miglitol

Miglitol ni dawa inayotumika kushusha kiwango cha sukari kwenye damu na kuhakikisha inabaki kwenye kiwango cha kawaida. Dawa hii iliyo kwenye kundi la dawa la alfa glukosidazi inhibita, hutumika pamoja na lishe sahihi na mazoezi ili kudhibiti kiwango cha sukari kwenye damu kwa wagonjwa wanaosumbuliwa na kisukari aina ya pili.

Acebutolol

Acebutolol

Acebutolol ni dawa mojawapo ya kutibu shinikizo la juu la damu iliyo kwenye kundi la dawa linaloitwa beta bloka. Dawa hii iliyo maarufu pia kwa jina la Sectral huwa na rangi nyekundu japo mara nyingi rangi ya dawa hutegemea na aina ya kiwanda.

Labetolol

Labetolol

Labetalol ni dawa mojawapo ya kutibu shinikizo la juu la damu iliyo katika kundi la dawa linaloitwa beta bloka na alfa bloka. Dawa hii huwa maarufu pia kwa jina la Trandate.

Nadolol

Nadolol

Nadolol ni dawa mojawapo ya kutibu shinikizo la juu la damu iliyo katika kundi la dawa linaloitwa beta bloka. Dawa hii huwa maarufu pia kwa jina la Corgard.

Atenolol

Atenolol

Atenolol ni dawa mojawapo ya kutibu shinikizo la juu la damu iliyo katika kundi la dawa zinazoitwa beta bloka.

Clozapine

Clozapine

Clozapine ni dawa kizazi kipya katika kundi la dawa za atipiko antisaikotiki, dawa hii hufahamika kama serotonini na dopamine inhibita kwa kuwa huzuia ufanyaji kazi wa homoni ya serotonin na dopamine kwenye mfumo wa kati wa fahamu ili kuleta madhara ambayo ndo kiini cha tiba yake

Hujapata dawa unayotafuta?

 

Endapo hujapata dawa unayotafuta andika katika kiboksi kilichoandikwa  "Tafuta chochote hapa...." juu ya kurasa hii na endapo hujapata katika kiboksi hiko basi wasiliana na wafamasia wa ULY CLINIC maelezo zaidi kuhusu dawa.

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri na tiba kwa kubofya linki ya 'Mawasiliano yetu' au 'Pata tiba' chini ya tovuti hii

bottom of page