Dawa
ULY CLINIC inakutahadharisha kuwa matumizi ya dawa pasipo ushauri wa daktari yanaweza kuleta madhara makubwa mwilini mwako.
Siku zote wasiliana na daktari wako kwa elimu na ushauri wa dawa gani na namna ya kutumia dawa inayoendana na hali yako halisi kama mbadala ya kujichukulia hatua mwenyewe.
​
Bonyeza 'Soma zaidi ' kwenye dawa unayohitaji kuanza kusoma kuhusu dawa hiyo..

Dawa ya kutostahimili laktosi
Kutostahimili laktosi kwa jina la kiingereza lactose intolerance ni tatizo linalotokea endapo tumbo linashindwa kumeng’enya sukari ya laktosi inayopatikana kwenye maziwa au mazao ya maziwa. Tatizo hili hupelekea mtu kupata, maumivu ya chembe ya moyo (kiungulia), kuharisha na dalili zingine(soma kwa maelezo zaidi Makala hii sehemu nyingine kwenye tovuti ya ULY CLINIC). Matibabu huhusisha kuepuka maziwa, kutumia maziwa yaliyopunguzwa au kutolewa kabisa laktosi au kutumia baadhi ya dawa ambazo huwa na kimeng’enya cha laktosi.

Dawa za kutibu na kukinga maambukizi ya TB
TB ni ugonjwa wa mapafu unaosumbua sana watu wengi duniani, historia zinaonyesha ugonjwa huu ulikuwa unaua kila mtu aliyeupata na dawa haikuwepo. Katika miaka ya 1882, Dr. Robert Koch aligundua bakteria anayesababisha TB na mwanga wa wanasayansi kuweza kugundua dawa. Toka mwaka huo TB imekuwa ikitibiwa bila mafanikio makubwa mpaka miaka ya 1940 ambapo dawa za TB zilianza kugunduliwa. Makala hii imezungumzia kuhusu dawa za kutibu na kujikinga na TB. Kumbuka dawa hizi hutumika kwa muunganiko, dawa moja huwa haina uwezo peke yake kutibu ugonjwa wa TB.
Hujapata dawa unayotafuta?
Endapo hujapata dawa unayotafuta andika katika kiboksi kilichoandikwa "Tafuta chochote hapa...." juu ya kurasa hii na endapo hujapata katika kiboksi hiko basi wasiliana na wafamasia wa ULY CLINIC maelezo zaidi kuhusu dawa.
​
Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri na tiba kwa kubofya linki ya 'Mawasiliano yetu' au 'Pata tiba' chini ya tovuti hii










