top of page

Mwandishi:

Dkt. Benjami L, MD

Mhariri:

Dkt. Salome A, MD

24 Aprili 2024 16:58:28

Image-empty-state.png

Kifafa kwenye ujauzito

Je degedege/kifafa kinaathari kwenye ujauzito?

Kifafa huwa hakina hakidhuru uwezo wa kupata mimba. Hata hivyo, matibabu ya kifafa huweza kudhuru mimba iliyotungwa. Dawa za kifafa kama Phenobarbital, phenytoin na carbemazepine huchakatwa kwenye vimengenya vya ini. Kwenye Mchakato wa umengenyaji huongeza uzalishaji wa protini zinazoshika homoni za jinsia na kusababisha zisifanye kazi. Hiyvo matumizi ya dawa za uzazi wa mpango kwa mtu anayetumiwa dawa za kifafa zinaweza zisilete matokeo yaliyokusudiwa kuzuia ujauzito. Wanawake wanaotumia dawa za kifafa wanatakiwa kutumia njia za vizuizi au kondomu badala ya dawa za uzazi wa mpango.

Je ujuzito unaongezaje kutokea kwa dalili za kifafa?

 

Dalili za kifafa hutokea sana wakati wa ujauzito kati ya asilimia 25 na 50 ya wanawake wenye kifafa kisichofahamika kisababishi chake. Kifafa kimekuwa kikiamka katika miezi mitatu ya kwanza ya ujauzito. Asilimia ya wanawake waliobakia huwa hawapati mabadiliko kipindi cha ujauzito na wakati si wajawazito. Wagonjwa wenye kifafa mara kwa mara kabla ya ujauzito huwa hatarini kushindwa kudhibiti kifafa hicho wakati waujauzito. Vivyo hivyo, kudhibiti kifafa kabla ya ujauzito huweza kusababisha kifafa kisiamke sana wakati wa ujauzito.

 

Nini husababisha kuamka kwa kifafa wakati wa ujauzito?

 

Sababu hazifahamiki vizuri, hata hivyo visababishi vinaweza kuwa

 • Kutodhibiti vema kwa kifafa kabla ya kupata ujauzito,

 • Ushauri duni au kutopata ushauri kuhusu ujauzito na kifafa,

 • Kutozingatia masharti ya dawa na

 • Kuwa ba kiwango kidogo cha dawa za kifafa kwenye damu wakati wa ujauzito.

 

Kumbuka; kuamka kwa kifafa wakati wa ujauzito hakumaanishi ujauzito utaofuata kitaamka pia.

 

Kifafa cha ujauzito kinamaanisha nini?

Cha kushangaza, kifafa kisichojulikana kisababishi hutambuliwa wakati wa ujauzito. Asilimia 25 ya wanawake wanaogunduliwa kwa mara ya kwanza kupata kifafa hiki hujulikana kuwa wana “kifafa cha ujauzito” wanaopata dalili wakiwa wajawazito tu. Kuamka kwa kifafa wakati wa ujauzito tu hakutabiri hatari kuamka kwa kifafa kwenye ujauzito ujao.

 

Kifafa kinadhuru vipi ujauzito?

 

Tafiti tofauti  zinaonyesha madhara ya kifafa kwenye ujauzito kuongeza hatari ya kusababisha mambo yafuatayo:

 • Kifafa cha mimba

 • Uchungu kabla ya wakati

 • Mtoto kuzaliwa amekufa

 

Hata hivyo tafiti zingine zimeshindwa kuonyesha uhusiano huu, kutokwa damu ukeni ni dalilii inayotokea mara kwa mara kwa wanawake wenye kifafa kwa sababu ya madhara ya dawa za kifafa zinazopunguza kiwango cha vitamin K kwenye damu.

Dawa gani za kifafa hutumika sana wakati waujauzito?

 

Phenytoin, Phenobarbital na carbamazepine hutumika sana kuliko primidone au valproic acid. Kila dawa inamadhara yake Fulani kwa mtoto hata hivyo, matumizi ya dawa moja huchaguliwa zaidi kuliko muunganiko wa dawa nyingi.

 

Ujauzito unaathiri vipi kiwango cha dawa za kifafa kwenye damu?

 

Kiwango cha chini cha dozi ya dawa Phenytoin, Phenobarbital na carbamazepine hutokea kwa sababu ya kuongezeka mwilini kwa majimaji ya damu (plazma) wakati wa ujauzito, kupungua kwa ufyonzaji na kuongezeka kwa umengenywaji wa dawa hizi kwenye ini kunakohusiana na ujauzito.


Kutumia vidonge vya folic asid wakati wa ujauzito pia hupunguza kiwango cha dawa phenytoin kwenye plazma. Hata kama kiwango cha dawa kwenye plazma kitapungua, kiwango cha dawa kinachofanya kazi huongezeka kwa kuwa kiwango cha protini kwenye plazma hupungua wakati wa ujauzito. Hivyo ni jambo la msingi kiwango cha dawa kuwa kinapimwa mara kwa mara ili kuweza kurekebisha dozi inayotumiwa a mjamzito.

 

Matatizo gani ya mchakato wa seli huambatana na matumizi ya dawa za kifafa wakati wa ujauzito?

 

Madini ya folic asid yamekuwa yakijulikana kupunguza uwezekano wa kupata watoto wenye matatizo kwenye mfumo wa fahamu kama kuzaliwa na mgongo wazi. Wanawake walio hatarini kupata watoto walio na mgongo wazi ni wale wanaotumia dawa za kifafa, hivyo hutakiwa kuongeza kiwango cha madini folic asid mpaka gramu 4 kwa siku badala ya dozi ya kawaida. Hata hivyo bado haijatiliwa mkazo kwamba folic asidi inaweza kuzuia madhara ya kupata mgongo wazi kutokana na dawa za kifafa.

Folic asidi hupunguza kiwango cha dawa phenytoin kwenye damu. Kwa hivyo kiwango cha dawa hii kinatakiwa kupimwa kwa wanawake wanaotumia folic asidi na dawa hii.

Dawa gani ya kifafa ni salama wakati wa ujauzito?

 

Kwa ujumla hakuna  dawa ya kifafa ambayo ni salama wakati wa ujauzito. Hata hivyo, kifafa kisipodhibitiwa huwa hatari kwa uhai wa mama na mtoto. Ili mama na mtoto kuwa salama waapaswa kutumia dawa hizii na kufanyiwa uchunguzi. Uchaguzi wa dawa hutegemea mtu na mtu.

 

Maelezo muhimu

 

 • Dawa za kifafa hutakiwa kutumiwa kabla ya kubeba mimba na dozi ifaayo iwe imetambuliwa, dawa moja na dozi ndogo hufaa.

 • Madini ya folic asid gramu 4 kwa siku yameonekana kupunguza hatari ya kupata watoto wenye migongo wazi kwa wanawake wanaotumia dawa za kifafa.

 • Hatari ya kupata watoto wenye matatizo ya kimaumbile huongezeka mara 2-3 kwa wanawake wanaotumia dawa za kifafa ukilinganisha na wale wasio na kifafa. Hata hivyo kutotumia kabisa dawa kwa wanawake wenye kifafa hatari huwa mara dufu zaidi.

Kuna dawa ya kifafa ambayo ni marufuku kutumia wakati wa ujauzito?

 

Ndio dawa aina ya trimethadione. Dalili za matumizi ya trimethadione ni kuchelewa kukua kwa mtoto, masikio kuwa chini zaidi, matatizo ya paa la kinywa, mpangilio mbaya wa meno, kushindwa kuongea, kuwa mfupi,kudumaa tumboni, matatizo ya moyo, macho, ubongo nje, kutofunguka kwa njia ya mkojo kwenye ncha ya uume. 2/3 ya watoto waliokuwa tumboni kwa mama aliyetumia dawa hii ya kifafa huwa na dalili mojawdaliliivyo mtumizi ya dawa hii yamekatazwa kabisa.

 

 

Madhara gani ya dawa za Phenytoin, Phenobarbital na carbamazepine?

 

Phenytoin

Madhaifu katika fuvu la kichwa na miguu, kutumia dawa hii pamoja na zingine za kifafa huweza kusababisha kupata mtoto mwenye ubongo nje, asiyekuwa ,kutofanyika vema sehemu ya kati ya uso na vidole.

 

Phenobarbital- Ingawa imekuwa ikihusianishwa na baadhi ya matatizo ya kuzaliwa kwa mtoto, hatari yake ni kumfanya mtoto kuwa teja na kupata dalili za kuacha dawa hizo.

 

Carbamazepine- Imekuwa ikionekana kuwa salama kuliko dawa zingine wakati wa ujauzito. Hata hivyo tafiti za karibuni zimehusisha kuongezeka kwa matatizo ya fuvu na uso, kuchelewa kukua na mgongo wazi.


Valproic asidi- Ni sumu kwa mtoto wakati wa ujauzito inayosababisha kuzaa mtoto mwenye matatizo ya moyo, kinywa, miguu na kikubwa ni mgongo wazi. Mama akitumia kwenye wiki ya 17 hadi 30 baada ya kupata ujauzito hatari ya mgongo wazi huwa ni asilimia 1-2. Wanwake wanaotumia dawa hii wakati wa hali mbaya zaidi wanatakiwa wafanyiwe uchunguzi wa karibu.

Kumbuka, unaweza kusoma zaidi kuhusu dawa salama kipindi cha ujauzito kwenye makala zetu zingine

Mtoto wa mama mwenye kifafa ana hatari ya kupata kifafa?

 

Mtoto anayezaliwa na mama aliyepata kifafa wakati wa ujauzito wake ana asilimia 3 ya kupata kifafa. Hatari inaweza kuwa kubwa kama kifafa hakifahamiki kisababishi, mama ameathiriwa au mtoto anapata degedege la homa.

Je mama mwenye kifafa na anatumia dawa za kifafa hatakiwi kumnyonyesha mtoto?

 

Hapana. Dawa za kifafa hupita kwa kiasi kidogo na kuingia kwenye maziwa na kiwango hiko hakina madhara kwa mtoto, hata hivyo mkusanyiko mkubwa wa dawa Phenobarbital na primidone ambayo huchakatwa kuwa Phenobarbital huweza kusababisha uchovu, kutonyonya vema na kuongezeka uzito kiasi. Kama haya yakitokea unyonyeshaji wa chupa unatakiwa kufanyika. Kunyonyesha hakuongezi hatari ya kupata degedege kwa mama.

  

Dawa mpya za felbamate, gabapentine na lamotrigine hazishauriwi kutumika wakati wa kunyonyesha kwa sababu hakuna ushahidi dhidi ya usalama wa dawa hizo.

 

Kwa taarifa zingine muulize daktari wako au wasiliana na daktari wako au tutafute kupitia mawasiliano yetu yaliyo katika mtandao huu

 

ULY Clinic inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchuku hatua yoyote ile inayohusu afya yako.

Wasiliana na daktari wa ULY Clinic kwa elimu zaidi na Tiba kwakubonyeza Pata Tiba au kupiga namba za simu chini ya tovuti hii.

​​

Bonyeza kusoma makala zingine zaidi kuhusu;

ULY Clinic inakushauri uwasiliane na daktari wako siku zote kabla ya kufanya maamuzi yanayohusisha afya yako
Wasiliana na daktari wa  ULY Clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kutumia namba za simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

24 Aprili 2024 16:58:28

Rejea za dawa

 1. Risks during pregnancy. Epilepsy Foundation. http://www.epilepsy.com/learn/impact/reproductive-risks/risks-during-pregnancy. Imechukuliwa 30.11.2020

 2. Frequently asked questions. Pregnancy FAQ129. Seizure disorders in pregnancy. American College of Obstetricians and Gynecologists. http://www.acog.org/~/media/For%20Patients/faq129.pdf?dmc=1&ts=20140521T1342401418. Imechukuliwa 30.11.2020

 3. Gabbe SG, et al. Neurological disorders in pregnancy. In: Obstetrics: Normal and Problem Pregnancies. http://www.clinicalkey.com. Imechukuliwa 30.11.2020

 4. https://www.epilepsy.com/learn/about-epilepsy-basics/what-epilepsy. https://www.epilepsy.com/learn/about-epilepsy-basics/what-epilepsy. Imechukuliwa 30.11.2020

bottom of page