top of page

Imeandikwa na ULY CLINIC

Maswali na majibu 1,000

Majibu ya kitaalamu ya maswali 1000 ya kiafya yaliyoulizwa kwa daktari wa ULY CLINIC

Karibu katika kurasa huu, katika kurasa hii utasoma kiundani kuhusu majibu ya maswali 100 yaliyoulizwa kwa daktari wa ULY CLINIC

1. Dalili za UTI

 

Katika makala hii, UTI linatumika kama neno tiba linalomaanisha Urinary tract Infection. Haya ni maambukizi yanayotokea katika mfumo wa mkojo.

Mfumo wa mkojo umegawanyika katika sehemu kuu mbili, mfumo wa chini ya mfumo wa juu.

Dalili za UTI katika mfumo wa juu wa mkojo huwa ni

 • Maumivu chini kidogo ya mbavu na upande wa kushoto na au kulia

 • Homa kali

 • Kukojoa damu au mkojo mchafu

 • Kutetemeka mwili

 • Kichefuchefu na kutapika

Dalili za UTI katika mfumo wa chini wa mkojo ni pamoja;

 • Kuungua wakati wa kukojoa

 • Kukojoa mara kwa mara bila kupitisha mkojo wa kutosha

 • Kuongezeka hamu ya kukojoa

 • Kukojoa damu

 • Mkojo kuwa na ukungu

 • Mkojo kuwa na rangi ya kokakola

 • Kukojoa mkojo wenye harufu mbaya

 • Maumivu ndani ya via za nyonga kwa wanawake

 • Maumivu ndani ya kifuko cha kinyesi kwa wanaume

Soma zaidi kuhusu  maambukizi ya UTI, dalili za UTI, dawa za kutibu UTI.

2. Makundi ya vyakula

 

Kuna aina tano za makundi ya vyakula, aina hizi 5 za makundi ya vyakula humwongoza mtu kupata afya njema ya mwili na kiakili pia. Makundi hayo ni;

 

 • Matunda

 • Mboga mboga

 • Wanga

 • Protini

 • Maziwa

3. Kuuma kwa chuchu ni dalili ya mimba?

 

Maumivu ya chuchu/titi ni moja kati ya dalili za mapema za ujauzito, huweza kutokea wiki la kwanza au la pili toka umepata ujauzito. Hata hivyo si kila maumivu ya chuchu husabaishwa na ujauzito. . Sababu zingine zinazoweza kupelekea maumivu ya chuchu ni maambukizi ya titi wakati wa ujauzito au baada ya kujifungua, komahedhi, na maumbile ya titi.

 

Soma zaidi kuhusu maumivu ya chuchu

 

4. Dawa ya kuzuia kutapika

 

Yapo makundi mbalimbali ya dawa zinazozuia kutapika, baadhi ya dawa zinazozuia kutapika ni;

 • Promethazine (phenergan)

 • Prochlorperazine(compazine)

 • Metoclopramide(reglan)

 • Diphenhydramine

Soma zaidi kuhusu  Dawa za kuzuia kutapika

 

5. Kifua kubana

 

Kifua kubana ni dalili kuu inayomaanisha kutumika sana kwa misuli au majeraha kwenye misuli, asilimia 20 hadi 49 ya kisababishi cha kifua kubana huletwa na matatizo ya isuli ya kifua. Haya huweza kutokea kwa sababu ya kuitumikisha misuli, uchovu mkuuu wa mwili au kuitumia misuli ndivyo sivyo. Kutumika sana kwa misuli ya kifua huleta dalili za kifua kubana. Sababu zingine zinazoweza kuchangia kifua kubana ni pamoja na;

 

 • Maambukizi ya COVID 19

 • Nimonia

 • GERD

 • Madhaifu ya Ang'zayati

 • Pumu ya kifua

 • Vidonga vya tumbo

 • Henia ya hayatazi

 • Kuvunjika kwa mbavu

 • Maambukizi ya herpes zosta kwenye ngozi(shingoz)

 • Mawe kwenye kifuko cha nyongo

 • Pankriataitizi

 • Shinikizo la juu la damu kwenye mapafu

 • Magonjwa ya mishipa ya damu ya moyo

 • Kostokondraitizi

 • Madhaifu ya mojongeo ya misuli ya esofagasi

 • Kuchanika kwa esofagasi

Soma zaidi kuhusu makala hii bonyeza maumivu ya kifua, kifua kuuma. maumivu ya kifua kutokana na moyo

6. Kukojoa mara kwa mara

 

Kukojoa mara kwa mara ni dalili inayoweza kusabbishwa na sababu zilizo za kawaida au magonjwa. Daktari wako atakuuliza kuhusu ni wakati gani unakojoa sana, wakati wa mchana, usiku au wakati wote. Majibu yako yatamsaidia kujua sababu halisi. dalili zinazoweza kuambatana na dalili hii huwa pamoja na maumivu wakati wa kukojoa, kuhisi kubakisha mkojo unapomaliza kukojoa, kuhisi kuungua wakati wa kukojoa, kubadilika kwa rangi ya mkojo, kushindwa kudhibiti mkojo kutoka. Kila dalili humaanisha tatizo fulani. Onana na daktari wako umwelezee ili ajue tatizo lako ni nini

 

Sababu zinazopelekea kukojoa mara kwa mara ni kama vile;

 

 • Henia ya kibofu cha mkojo(sistosili)

 • Madhaifu ya ang'zayati

 • Kuvimba kwa tezi dume

 • Mawe kwenye kibofu cha mkojo

 • Kisukari cha maji

 • Kisukari aina ya kwanza na pili

 • Kutumia dawa za kupunguza maji kama diuretics

 • Maambukizi ya UTI

 • Maambukizi kwenye figo

 • Kufanya kazi kusiko kawaida kwa kibofu cha mkojo

 • Ujauzito

 • Maambukizi kwenye tezi dume

 • Maambukizi ukeni

 • Makovu ndani ya mrija wa urethra

Soma zaidi makala hii kwa kubonyeza "kukojoa mara kwa mara"

7. Dalili za upungufu wa damu

Upungufu wa damu hutokea pale unapokosa kiwango cha kutosha cha chembe nyekundu za damu. Kwa jina jingine, dalili hii hufahamika kama anemia. Baadhi ya dalili kuu zinazoambatana na upungufu wa damu ni;

 • Uchovu wa mwili

 • Kuchoka kupita kiasi

 • Kupauka kwa ngozi au manjano

 • Mapigo ya moyo kwenda isivyo kawaida

 • Kuhisi mapiga ya moyo(moyo kwenda kasi au taratibu)

 • Kuishiwa pumzi

 • Kuhisi kizunguzungu

 • Kuhisi kichwa chepesi

 • Maumivu ya kifua

 • Kupoa kwa miguu na mikono

 

Bonyeza dalili za upungufu wa damu kusoma zaidi

8. Macho

Bonyeza kusoma kuhusu majibu ya maswali yaliyoorodheshwa hapa chini kuhusu macho;

9. Ulimi

Maswali na majibu kuhusu ulimi, bonyeza hapa kusoma

Imeboreshwa mara ya mwisho 1.11.2020

bottom of page