top of page

Mwandishi:

Mhariri:

Imeboreshwa:

ULY CLINIC

ULY CLINIC

Kupoteza uwezo wa kutamka maneno
shahawa-zenye-damu-ulyclinic-compressor.

6 Aprili 2026, 12:18:28

Kupoteza uwezo wa kutamka maneno

Disarthria ni hali ya kushindwa kutamka vema maneno, hali hii huambatana na kutamka maneno taratibu na kwa tabu bila mpangilio unaotakiwa.


Pia huweza kuambatana na utumiaji wa sauti kutoka puani endapo kisababishi ni tatizo kwenye ukuta wa palate. Mara nyingi inaweza kuchanganywa na neon aphasia, ambapo mtu anapoteza uwezo wa kuongea au kutengeneza maneno.


Dysarthria hutokana na kuharibiwa kwa sehemu ya shina la ugondo inayopelekea kuleta udhaifu kwenye mishipa ya neva ya cranial namba IX, X na XII inayohusika kuongoza kiboksi cha kutengeneza sauti.


Visababishi

  • Kuisha kwa cerebella kutokana na matumizi sugu ya pombe

  • Kutojitosheleza kwa mshipa wa damu wa basilar

  • Botulism

  • Majeraha ya kichwani

  • Kunywa sumu ya mercury

  • Ugonjwa wa multiple sclerosis

  • Ugonjwa wa Parkinson’s

  • Ugonjwa wa myasthenia gravis

  • Kiharusi kwenye ubongo wa kati na shina la ubongo

  • Kuzidisha dozi ya dawa za kutibu au kuzuia degedege

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii

Imeandikwa:

2 Aprili 2026, 15:59:23

Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini

​

[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]

Rejea za mada

bottom of page