top of page

Dawa

ULY CLINIC inakutahadharisha kuwa matumizi ya dawa pasipo ushauri wa daktari yanaweza kuleta madhara makubwa mwilini mwako.

 

Siku zote wasiliana na daktari wako kwa elimu na ushauri wa dawa gani na namna ya kutumia dawa inayoendana na hali yako halisi kama mbadala ya kujichukulia hatua mwenyewe.

Bonyeza 'Soma zaidi ' kwenye dawa unayohitaji kuanza kusoma kuhusu dawa hiyo..

Tolazamide

Tolazamide

Tolazamide ni dawa inayotumika katika matibabu ya kisukari na ipo kwenye kundi la kizazi cha kwanza cha dawa za sulfonylurea.

Metformin

Metformin

Ni dawa mojawapo iliyo kwenye kundi la Biguanide, hutumika kutibu ugonjwa wa kisukari aina ya pili. Dawa hii huuzwa sana/ hufahamika kwa jina la Glucophage.

Fluoride

Fluoride

Floraidi (fluoride) ni madini yanayohifadhiwa kwa wingi kwenye meno na mifupa. Madini haya hutumiwa na wataalamu wa meno kuimarisha ukuta wa meno uitwao enemo ili usishambuliwe na vimelea wa meno.

Sodium

Sodium

Sodium ni moja madini muhimu sana mwilini. Upungufu wa sodium huweza kusimamisha shughuli nyingi ndani ya mwili, mfano shughuli za usafirishaji wa taarifa kati ya mishipa ya fahamu, ubongo na moyo.

Mefenamic acid

Mefenamic acid

Ni dawa jamii ya NSAIDs inayozuia inflamesheni kwenye seli hivyo kuleta madhara chanya ya kuzuia uvimbe, kutuliza maumivu na homa.

Ziprasidone

Ziprasidone

Ni dawa mojawapo ya kizazi cha pili katika kundi la dawa antisaikotiki (kundi hili hufahamika pia kama atipiko antisaikotiki ). Dawa hii huwa na maudhi kidogo kulinganisha na dawa zingine kwenye kundi hili, pia huwa na uwezo sawa na dawa za antisaikotiki kizazi cha kwanza.

Oxaprozin

Oxaprozin

Ni dawa jamii ya NSAIDs inayotumika kutuliza au kuzuia uvimbe kutokana na michomo kinga, kutuliza maumivu na homa.

Olanzapine

Olanzapine

Ni dawa ya kutibu magonjwa ya akili, iliyo kwenye kundi la antisaikotiki. Baadhi ya magonjwa hayo ni magonjwa ya schizophrenia na baipola.

Natalizumab

Natalizumab

Ni dawa iliyo kwenye kundi la dawa la monoklono antibodi, hufanya kazi kwa kuzuia chembe za damu za lyukosaiti kuingia kwenye mfumo wa fahamu wa kati na hivyo kupunguza inflamesheni na kuondolewa kwa mayelini za mishipa ya fahamu.

Naproxen

Naproxen

Ni dawa jamii ya NSAIDs inayozuia inflamesheni kwenye seli hivyo kuleta madhara chanya ya kuzuia uvimbe, kutuliza maumivu na homa.

Meclofenamate

Meclofenamate

Ni dawa jamii ya NSAIDs inayozuia inflamesheni kwenye seli hivyo kuleta madhara chanya ya kuzuia uvimbe, kutuliza maumivu na homa.

Doravirine

Doravirine

Doravirine ni dawa ya kufubaza makali ya virusi vya UKIMWI iliyo kwenye kundi la dawa zinazoitwa NNRTIs.

Hujapata dawa unayotafuta?

 

Endapo hujapata dawa unayotafuta andika katika kiboksi kilichoandikwa  "Tafuta chochote hapa...." juu ya kurasa hii na endapo hujapata katika kiboksi hiko basi wasiliana na wafamasia wa ULY CLINIC maelezo zaidi kuhusu dawa.

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri na tiba kwa kubofya linki ya 'Mawasiliano yetu' au 'Pata tiba' chini ya tovuti hii

bottom of page