top of page

Dawa

ULY CLINIC inakutahadharisha kuwa matumizi ya dawa pasipo ushauri wa daktari yanaweza kuleta madhara makubwa mwilini mwako.

 

Siku zote wasiliana na daktari wako kwa elimu na ushauri wa dawa gani na namna ya kutumia dawa inayoendana na hali yako halisi kama mbadala ya kujichukulia hatua mwenyewe.

Bonyeza 'Soma zaidi ' kwenye dawa unayohitaji kuanza kusoma kuhusu dawa hiyo..

Bisoprolol

Bisoprolol

Bisoprolol ni ya dawa mojawapo ya kutibu shinikizo la juu la damu iliyoko katika kundi la dawa linaloitwa beta bloka. Dawa hii huwa maarufu pia kwa jina la Zebeta au Monocor.

Reserpine

Reserpine

Reserpine ni dawa ya kutibu shinikizo la juu la damu iliyo kundi la Rauwolfia alkaloid. Dawa hii hutokana na mizizi ya mmea unaoitwa Rauwolfia serpentine na vomitoria.

Rosiglitazone

Rosiglitazone

Rosiglitazone ni dawa mojawapo ya kutibu kisukari aina ya pili iliyopo kwenye kundi la thiazolidinedione.

Bosentan

Bosentan

Bosentan ni dawa ya kutibu shinikizo la juu la damu kwenye mishipa ya palimonari iliyopo kwenye kundi la Endothelin Receptor Antagonisti. Dawa hii huwa maarufu kwa jina la Tracleer.

Erythromycin

Erythromycin

Erythromycin yenye jina jingine la ery-ped, ni dawa jamii ya antibayotiki inayotumika kutibu maambukizi yanayosababishwa na bakteria iliyo kwenye kundi la macrolide inayozalishwa kutokwa kwa bakteria anayeitwa Saccharopolyspora erythraea.

Azithromycin

Azithromycin

Azithromycin yenye jina jingine la Zithromax au AZUMA, ni dawa jamii ya antibayotiki inayotumika kutibu maambukizi yanayosababishwa na bakteria iliyo kwenye kundi la macrolide. Dawa hii hupatikana katika mfumo wa kidonge, tembe na kimiminika kwa ajili ya kunywa au kutumika kwa kuchoma sindano.

Betaxolol

Betaxolol

Betaxolol Ni aina ya dawa mojawapo ya kutibu shinikizo la juu la damu iliyoko katika kundi la dawa linaloitwa beta bloka. Dawa hii huwa maarufu pia kwa jina la Kerlone.

Carvedilol

Carvedilol

Carvedilol ni dawa mojawapo ya kutibu shinikizo la juu la damu iliyoko katika kundi la dawa linaloitwa beta bloka. Dawa hii huwa maarufu pia kwa jina la Coreg.

Troglitazone

Troglitazone

Troglitazone ni dawa mojawapo iliyokuwa ikitumika kutibu ugonjwa wa kisukari aina ya pili iliyopo kwenye kundi la dawa linaloitwa thiazolidinedione. Dawa hii huwa maarufu kwa jina Rezulin na hupatikana katika mfumo wa kidonge.

Amiloride

Amiloride

Amiloride ni dawa mojawapo ya kutibu shinikizo la juu la damu Iliyo kwenye kundi la dawa linaloitwa Potasiamu sparing diuretic. Dawa hii huwa maarufu kwa jina la Midamor.

Triamterene

Triamterene

Triamterene ni dawa mojawapo ya kutibu shinikizo la juu la damu iliyo kwenye kundi la dawa linaloitwa Potasiamu sparing diuretic.

Spironolactone (Aldactone)

Spironolactone (Aldactone)

Spironolactone ni dawa mojawapo inayotumika kushusha shinikizo la juu la damu iliyo kundi la Potasiamu sparing diuretic.

Hujapata dawa unayotafuta?

 

Endapo hujapata dawa unayotafuta andika katika kiboksi kilichoandikwa  "Tafuta chochote hapa...." juu ya kurasa hii na endapo hujapata katika kiboksi hiko basi wasiliana na wafamasia wa ULY CLINIC maelezo zaidi kuhusu dawa.

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri na tiba kwa kubofya linki ya 'Mawasiliano yetu' au 'Pata tiba' chini ya tovuti hii

bottom of page